Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waethiopia 25 washikiliwa Kilimanjaro
Habari Mchanganyiko

Waethiopia 25 washikiliwa Kilimanjaro

Spread the love

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia raia 25 wa Ethiopia waliongia nchini bila ya kufuata sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waethiopia hao ambao tisa kati yao ni watoto wenye umri chini ya miaka 18, walikamatwa na polisi wakiwa katika kichaka eneo la Himo wakisubiri gari kwa ajili ya kuwavusha kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini.

Kamishna Maidizi wa Polisi Hamis Issah, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,amesema raia hao wa Ethiopia walikamatwa na askari Polisi wakati wa doria wakiwa na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Baraka Itema (25) aliyejitambulisha kama fundi ujenzi .

Kamanda Issah amesema Waethiopia hao wanaendelea kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kusaidiana na jeshi la polisi na kwamba mara baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingia nchini bila ya kibali.

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!