Mchungaji kutoka kanisa la Waamini la nchini Marekani, Dana Morey (kushoto)

Wachungaji Marekani, Rwanda waombea corona wakiwa Tanzania

Spread the love

WACHUNGAJI kutoka nchi za Marekani na Rwanda wameahidi kuombea nchi zao na nyingine kuondokana na janga la Ugonjwa wa Corona kupitia Tanzania kwa sababu nchi hii imekuwa ya pekee katika mataifa mbalimbali ambayo watu wake wanaendelea na kazi zao kama kawaida licha ya kuwepo na tishio la ugonjwa huo duniani. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea). 

Wachungaji hao akiwemo Mchungaji kutoka kanisa la Waamini la nchini Marekani, Dana Morey walisema hayo jana wakati wakiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa semina ya neno la Mungu katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege vilivyopo Manispaa ya Morogoro.

Mchungaji Morey alisema Tanzania ni nchi ambayo watu kutoka mataifa mbalimbali wanaiongelea kwa sababu ya kuwa na utulivu na watu wanatembea kwa uhuru katika nyakati hizi za corona kutokana na maombi ya siku tatu yaliyoongozwa na Rais John Magufuli ya kuondoa  ugonjwa huo.

“Nchi hii mnaonesha ni namna gani mnamjua Mungu, hakuna kiongozi yeyote aliyeweza haya kutoka nchi zingine, lakini Tanzania imetumia siku tatu kwa kusali na Mungu akakubali maombi yenu,” alisema mchungaji huyo.

Alisema wameamua kufika Morogoro  kama sehemu yao ya kwanza kutembelea Tanzania kutangaza neno la Mungu baada ya kuingia ugonjwa wa corona huku wakiwa na neno moja kwa wanadamu kuwa wamwamini Mungu kwa maana yeye anawapenda na ndio maana akamtoa mwanaye wa pekee afe msalabani ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.

Rais Magufuli na Viongozi wa Dini

Mchungaji huyo alisema kupitia maombi yanayoanza Septemba 10 hadi 13 watu watakaoshiriki watabadilisha maisha yao ikiwemo kuondoshwa kwa magonjwa yaliyowasumbua kwa muda mrefu na magumu mengine yaliyowasumbua kwa muda mrefu yote yatakwisha.

Naye Muinjilisti kutoka kanisa la Mwanga wa Mataifa la nchini Rwanda Dk. Lau Tumusime alisema Tanzania ndio nchi pekee ambayo inakubali mikutano na mikusanyiko na wananchi wanaitika kuomba.

Alisema wanakaribisha watu wote kwenye mkutano huo kwa sababu Mungu amepanga kuwaombea ambapo wameamua kutumia mwaka  2020/21 kwenda Tanzania baada ya Mungu kuwaelekeza kutoa huduma nchini humo.

Naye Mwenyekiti wa makanisa ya Pentekoste (TAG) mkoani Morogoro, Askofu Bryson Msuya, alisema katika semina hiyo pia watamwomba Mungu aivushe salama Tanzania katika kipindi cha uchaguzi, kupitia maombi ya amani na umoja yatakayoendelea wakati wa semina hiyo.

Alisema baraza la makanisa ya kipendekeste wanawapenda watu wote hivyo kudumisha amani na umoja hasa kipindi cha uchaguzi ni jambo jema ambalo watasimama nalo na Mungu kwa maombi.

Hivyo aliwaomba wananchi kujitokeza katika semina hiyo ya neno la Mungu itakayoanza saa tisa mchana huku Muimbaji wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozbert atakuwepo kuimba nyimbo za injili na waimbaji wengine sambamba na kuwepo kwa zawadi mbalimbali zitakazotolewa mwisho mwa mkutano kila siku zikiwemo friji na pikipiki.

WACHUNGAJI kutoka nchi za Marekani na Rwanda wameahidi kuombea nchi zao na nyingine kuondokana na janga la Ugonjwa wa Corona kupitia Tanzania kwa sababu nchi hii imekuwa ya pekee katika mataifa mbalimbali ambayo watu wake wanaendelea na kazi zao kama kawaida licha ya kuwepo na tishio la ugonjwa huo duniani. Anaripoti Christina Haule, Morogoro ... (endelea).  Wachungaji hao akiwemo Mchungaji kutoka kanisa la Waamini la nchini Marekani, Dana Morey walisema hayo jana wakati wakiongea na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa semina ya neno la Mungu katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege vilivyopo Manispaa ya Morogoro.…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Christina Haule

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!