Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge Z’bar walalamikia vikwazo vya biashara Bara
Habari za Siasa

Wabunge Z’bar walalamikia vikwazo vya biashara Bara

Spread the love

WABUNGE wa Zanzibar, wameonesha kukerwa na vikwazo vya ushuru wanavyopitia wafanyabiashara wanaoingiza na kusafirisha bidhaa zao nje ya nchi kupitia Tanzania Bara. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wakizungumza bungeni katika nyakati tofauti leo tarehe 30 Mei 2019, wabunge hao wamehoji sababu za bidhaa za Zanzibar ikiwemo za uvuvi zinazosafirishwa nje ya nchi, hupitia vikwazo vingi kulinganisha na bidhaa zinazotoka kwenye nchi jirani.

Jafu Hashim Ayub, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar (CCM) amedai kwamba, bidhaa za Zanzibar hupata vikwazo vingi zinapoingia Tanzania Bara  kulinganisha na bidhaa zinazoingia kutoka nchi jirani hasa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC).

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji amekanusha madai hayo akisema kwamba, bidhaa zote zinazoingia Tanzania Bara hufuata utaratibu wa forodha unaofanana.

Dk. Kijaji ameeleza kuwa, bidhaa za nchi wanachama wa EAC na SADC hupata msamaha wa ushuru wa forodha lakini hutozwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT.)

“Sio kweli kwamba bidhaa za Zanzibar zinapata usumbufu ukilinganisha na bidhaa za nchi jirani zinapoingia Tanzania Bara, kwa sababu zote zinafuata utaratibu wa forodha unaofanana.

Bidhaa zinazoingiza Tanzania Bara kutoka nchi wanachama wa EAC na Kusni mwa Afrika hupata msamaha wa ushuru w aforodha  bidhaa hupata msamaha wa ushuru wa forodha lakini hulipa VAT,”amesema Dk. Kijaji.

Haji Khatib Kai amelalamikia changamoto ya wakazi wa Zanzibar kupata vikwazo pindi wanapotaka kuingiza magari yao Tanzania Bara kutokea visiwani humo kwa ajili ya matumizi binafsi, akisema kwamba wamekuwa wakipitia vikwazo mbalimbali ikiwemo vya ushuru.

Akijibu swlai hilo, Dk. Kijaji amesema changamoto hiyo imesababishwa na tofauti za mifumo ya uthaminishaji mizigo kwa ajili ya kukadiria viwango vya kodi, na kwmaba sababu hiyo inapelekea mizigo ikiwemo magari yanayoptoka Zanzibar yakiingia Tanzania Bara yapimwe upya ili kujua kodi stahiki.

“Niliwaambia kwa nini tuko kwenye mkanganyiko huo, TRA huku Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanatumia mifumo tofauti ya uthaminishaji mizigo ndio maana lazima yafanyiwe uthamini upya ili kujua kodi stahiki, hilo lina fahamika vizuri, niombe tukubaliane na jambo hili ili tuondoke kwenye mkanganyiko huu,” amesema Dk. Kijaji.

Rukia Kassim Ahmed amehoji sababu za magari yanatoka visiwani Zanzibar yanapoingia Tanzania Bara hayawezi kupewa namba mpya za usajili hadi yalipie kodi.

Akijibu swlai hilo, Dk. Kijaji amesema changamoto hiyo pia inasababishwa na tofauti ya mfumo wa utozaji kodi ulioko baina ya Zanzibar na Tanzania Bara.

“Nimeshaeleza changamoto ya kimfumo tuliyo nao, unapopewa namba Tanzania Bara ubatumia Tanzania Bara, na utofauti wa kimfumo lazima tuitathimini na kuangalia utofauti wa kodi ili gari lako liweze kupata usajili,” amesema Dk. Kijaji.

Naye Machano Othman Said, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (CCM), amehoji sababu za bidhaa za uvuvi hasa dagaa zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia mpaka wa Tunduma hutozwa kiasi kikubwa cha kodi.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema serikali imefanya mabadiliko ya tozo mbalimbali za mazao ya mifugo na uvuvi na kwamba ifikapo tarehe Mosi Julai mwaka huu tozo hizo mpya zitaanza kutumika na kupunguza changamoto ya wafanyabiashara kushindwa kulipa ushuru.

“Kuhusu tozo kuonekana kubwa na kupelekea  kuwa juu ya uwezo wa wafanyabiashara na kushindwa kulipia, hapa karibuni wizara tulifanya mabadiliko ya tozo mbalimbali za mazo ya mifugo na uvuvi. Kuanzia tarehe 1 Julai tunayo matumaini tozo zitashuka na wafanyabiashara kusafirisha mazao ya mifugo kwenda nchi za nje,” amesema Ulega.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!