WABUNGE wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wametakiwa kufika Dodoma kwa ajili ya usajili unaoanza leo Jumamosi hadi tarehe 9 Novemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Kikao cha kwanza cha Bunge la 12, kitafanyika Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi tarehe 7 Novemba 2020 ofisi za bungeni, Dodoma amesema, “kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge jipya kitafanyika tarehe 10 Novemba 2020.”
Amesema, usajili na taratibu nyingine za kiutawala zitafanyika ofisi ya Bunge Dodoma.
Kagaigai amesema, wabunge wateule wote wanapaswa kufika wakiwa na nyaraka; hati ya kuchaguliwa/kuteuliwa kuwa mbunge na nakala ya kitambulisho cha Taifa.
Pia, Kadi ya Benki yenye namba ya akaunti ya mbunge; cheti cha ndoa kinachotambuliwa na Serikali (kwa wenye ndoa), cheti cha kuzaliwa cha watoto wenye umri chini ya miaka 18 (kwa wenye watoto), vyeti vya elimu/taaluma, nakala ya wasifu wa mbunge na picha (pasipoti size) nakala nane.
Leave a comment