Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ‘Wabunge wa Lipumba’ kikaangoni kesho
Habari Mchanganyiko

‘Wabunge wa Lipumba’ kikaangoni kesho

Wabunge wa CUF waliovuliwa uanachama wakiwa mahakamani wakisikiliza shauri lao la kupinga hatua hiyo
Spread the love

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam inatarajia kutoa uamuzi wa zuio jipya la kutoapishwa kwa Wabunge wateule wa upande wa Chama cha Wananchi – CUF unaumuunga Mkono Professa Ibrahim Lipumba, anaandika Faki Sosi.

Prof. Lipumba ni mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Leo wakili wa wabunge wa chama hicho waliofukuzwa uanachama na kambi ya Prof. Lipumba, Peter Kibatala mbele ya Jaji Lugani Mwandambo amewasilisha hoja za pingamizi hilo la muda.

“Mahakama kesho itatoa uamuzi wa zuio dogo la muda, juu mapingamizi tuliowasilisha ili wabunge walio ondolewa wabaki kama waliovyo na wale waliotangazwa na tume ya uchaguzi wasiapishwe.

“Tumekubaliana mapingamizi ya awali waliyoleta walalamikiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali yasikilizwe kwa maandishi na uamuzi juu yake utatoka tarehe 27 Agosti 2017,” amesema.

Mahakama itatoa uamuzi huo kesho saa 7:30 Mchana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!