Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge 90 CCM wafyekwa 
Habari za SiasaTangulizi

Wabunge 90 CCM wafyekwa 

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, ‘kimewakata’ wabunge wake zaidi ya 90 waliokuwa wakitetea nafasi zao ndani ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Baadhi ya wabunge waliokatwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli, walikuwa wameongoza kwenye kura za maoni.

Kati ya wabunge hao, walioangukia pua, wamo mawaziri wawili na naibu mawaziri wawili.

Mawaziri hao ni; Dk. Harrison Mwakyembe wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Angellah Kairuki wa Ofisi ya Waziri Mkuu –Uwekezaji.

Naibu mawaziri ni; Omar Mgumba wa Kilimo na Dk. Mary Mwanjelwa wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Kati ya wabunge 93, 88 ni wa majimbo, watatu wa viti maalum na wawili walikuwa viti maalum lakini walijitosa majimboni na kushindwa.

Ukiwaacha wabunge hao 93. Kuna wabunge wawili, Profesa Anna Tibaijuka wa Muleba Kusini na John Kadutu wa Ulyankulu wao walitangaza awali kustaafu kuwania ubunge huku Nimrod Mkono wa Butiama yeye hakujitosa kutokana na hali ya kiafya.

Andrew Chenge

Kwa hali hiyo, ukichukua hao 93 waliokatwa na watatu hawakujitosa kwenye mbio hizo, wanafika 96 ambao sura zao hazitoonekana ndani ya Bunge la 12 labda miongoni mwao wateulewe na Rais katika nafasi zake kumi za wabunge.

Baadhi ya wabunge hao waliofyekwa na majimbo yao pembeni ni;

  1. Dk. Charles Tizeba – Buchosa
  2. William Ngeleja – Sengerama
  3. Balozi Rajab Adad – Muheza
  4. Omar Mugumba – Morogoro Kusini Mashariki
  5. Balozi Diodorus Kamala – Nkenge
  6. Dk. Harrison Mwakyembe – Kyela
  7. Stephen Masele – Shinyanga Mjini
  8. Julius Kalanga – Monduli
  9. Maulid Mtulia – Kinondoni
  10. Abadallah Mtolea – Temeke
  11.  Lolesia Bukwimba – Busanda
  12.  Juma Nkamia – Chemba
  13. Chacha Ryoba – Serengeti
  14. Albert Obama – Buhigwe
  15. Daniel Nsanzugwanko – Kasulu Mjini
  16. Mbaraka Bawazir – Kilosa
  17. Goodluck Mlinga – Ulanga
  18. Suleiman Ahmed Saddiq -Mvomero
  19. Dk. Shukuru Kawambwa – Bagamoyo
  20. Dk. Haji Mponda – Malinyi
  21. Peter Lijualikali – Kilombero
  22. Victor Mwambalaswa – Lupa
  23. Haroon Pirmohamed – Mbarali
  24. Rafael Gashaza – Ngara
  25. Profesa Jumanne Maghembe – Mwanga
  26. Hassan Masala – Nachingwea
  27. Jitu Soni – Babati Mjini
  28. Isaay Paulo – Mbulu Mjini
  29. James Millya – Simanjiro
  30. Emmanuel Papian – Kiteto
  31. Omar Badwel – Bahi
  32. Issa Mangungu – Mbagala
  33. Augustino Masele – Mbogwe
  34. Venance Mwamoto – Kilolo
  35. Godfrey Mgimwa – Kalenga
  36. Mahmoud Mgimwa – Mufundi Kaskazini
  37. Edwin Sannda – Kondoa Mjini
  38. Charles Kitwanga – Misungwi
  39. Oscar Mukasa  – Biharamulo Magharibi
  40. Dk. Pundenciana Kikwembe – Kavuu
  41. Richard Mbogo – Nsimbo
  42. Christopher Chiza – Buyungu
  43. Peter Serukamba – Kigoma Kaskazini
  44. Profesa Norman Sigalla – Makete
  45. Kangi Lugola – Mwibara
  46. Deogratias Ngalawa – Ludewa
  47. Hassan Kaunje – Lindi Mjini
  48. William Dau – Nanyumbu
  49. Jerome Bwanausu – Lulindi
  50. Rashid Chuachua – Masasi
  51. Saul Amon – Rungwe
  52. Dk. Mary Nangu – Hanang
  53. Hasna Mwilima – Kigoma Kusini
  54. George Lubeleje – Mpwapwa
  55. Joel Mwaka – Chinolwa sasa linaitwa Chamwino
  56. Janet Mbene – Ileje
  57. Omary Kigoda – Handeni Mjini
  58. Mary Chatanda – Korogwe Mjini
  59. Mboni Mhita – Handeni Vijijini
  60. Edward Mwalongo – Njombe Mjini
  61. Joram Hongoli – Lupembe
  62. Greyson Lwenge – Wanging’ombe
  63. Dk. Dalaly Kafumu – Igunga
  64. Mussa Ntimizi – Igalula
  65. Ezekiel Maige – Msalala
  66. Andrew Chenge – Bariadi
  67. Dk. Raphael Chegeni – Busega
  68. Salum Khamis – Meatu
  69. Daniel Mtuka – Manyoni Mashariki
  70. Allan Kiula –Iramba Mashariki
  71. Justin Monko – Singida Kaskazini
  72. Sixtus Mapunda – Mbinga Mjini
  73. Mbaraka Dau – Mafia
  74. Edwin Ngonyani – Namtumbo
  75. Saada Mkuya – Welezo
  76. Martin Msuha – Mbinga Vijijini
  77. Ignas Malocha – Kwela
  78. Hamoud Jumaa – Kibaha Vijijini
  79. Ally Ungando – Kibiti
  80. Khamis Yahya Machano – Chaani
  81. Makame Mashaka Foum – Kijini
  82. Sadifa Juma Khamis – Donge
  83.  Bhagwanji Maganlal Meisuria – Chwaka
  84. Salum Mwinyi Rehani – Uzini
  85. Haji Amie Haji – Makunduchi
  86. Shamsi Vuai Nahodha – Kijitoupele sasa linaitwa Pangawe
  87. Kanali mstaafu Masoud Ali Khamis – Mfenesini
  88. Jamal Kassim Ali – Magomeni
  89. Angella Kairuki – Alikuwa viti maalum, akagombea Same Magharibi
  90. Halima Bulembo – Viti Maalum
  91. Dk. Mary Mwanjela – Viti Maalum
  92. Vick Kimata – alikuwa viti maalum, akagombea Kibamba
  93. Amina Mollel- Viti Maalum
Bunge la Tanzania

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!