May 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waandamanaji wamiminiwa risasi za moto Nigeria

Spread the love

NCHINI Nigeria, zaidi ya miili 20 imepatikana baada ya kumiminiwa risasi na jeshi la nchi hiyo kuwamiminia risasi waandamanaji wanaopinga ukatili wa polisi nchini humo. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Taarifa kutoka mashirika mbalimbali ya habari yanaeleza, watu zaidi ya 50 wamejeruhiwa wakati wanajeshi wakimimina risasi waandamanaji hao katika viunga kwa Lagos, Nigeria.

Mauaji hayo yamefanyika jana jioni Jumanne tarehe 20 Oktoba 2020, Lagos na wanaotajwa kuwa wanajeshi wa taifa hilo waliovalia kiraia.

Askari wenye silaha walikuwa wakiwazuia waandamanaji kabla ya risasi kuanza kurindima.

“Walikuwa wanapiga risasi moja kwa moja kwetu, lilikuwa tukio baya. Kuna mtu alipigwa risasi na kufa hapo hapo.

“Walipiga risasi kwa muda wa saa moja na nusu na baada ya hapo, askari walichukua miili ya waliouawa,” shuhuda mmoja aliiambia BBC.

Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji, hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeza kupata habari za kuaminika kuhusu vifo hivyo.

Taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) zimeeleza, maofisa wa jeshi Nigeria wameahidi kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo.

Katika Jiji la Lagos na maeneo mengine, wananchi wamepewa amri ya kutotoka nje. hata hivyo, waandamanaji wameendelea kujitokeza na kuzingira vituo vya polisi.

Kutokana na mapigano ya risasi yanayoendelea , Hillary Clinton, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marekani amemtaka Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari kuacha kuua vijana.

Odion Jude Ighalo, mcheza wa Manchester United, kupitia ukursa wake wa twitter ameishutumu Serikali ya Nigeria kwa kuua wananchi wake.

error: Content is protected !!