Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vyama, wagombea waonywa kutofanya haya
Habari za SiasaTangulizi

Vyama, wagombea waonywa kutofanya haya

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imebainisha mambo mbalimbali ambayo hayapaswi kufanywa na vyama vya siasa na wagombea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Makatazo hayo ni miongoni mwa maadili ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2020.

Baadhi ya mambo hayo yaliyozuiwa ni; kufanya fujo au kuchochea vurugu ya aina yoyote katika mikutano ya vyama vingine na kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na vitisho au lugha inayochochea uvunjifu wa amani au kuashiria ubaguzi wa kijinsia, ulemavu, rangu au maumbile kwenye mikutano na kwenye shughuli zote za kampeni.

Pia, kuwa na, au kubeba sananu, kinyago au kitu chochote ambacho kinaonesha kudhalilisha, kukebehi au kufedhehesha chama kingine cha siasa au kiongozi wake au Serikali katika mkutano au mkasanyiko wowote wa kisiasa.

Makatazo mengine ni; viongozi wa vyama vya siasa au wagombea na wafuasi wao kutumia vipaza sauti vya aina yoyote ile kwa shughuli za kisiasa nyakati zote za usiku kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 12:00 asubuhi.

Safu ya kuu ya uongozi ya Chama cha Demokrasja na Maendeleo (Chadema)

Mengine ni; viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo ya kampeni ya vyama vingine vya siasa na matangazo ya uchaguzi yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Pia, kubandika mabango ya kampeni, matangazo au michoro yoyote kwenye nyumba, majengo au vyombo vya usafiri vya watu binafsi au taasisi mbalimbali bila idhini ya wamiliki husika; kukosoana kati ya vyama na wagombea kunapofanyika inabidi kujikita katika sera, programu na kazi zao walizofanya. Ukosoaji wa vyama vingine au wagombea wengine kwa tuhuma zizizothibitishwa ni lazima uepukwe.

Wanachama wa ACT-Wazalendo, wakiwa kwenye mkutano Mlimani City

Mambo mengine ni; kuomba kupigiwa kura kwa misingi ya udini, ukabila, jinsia au rangi na vyama vya siasa, wagombea, wanachama au wafuasi wao kuzuia watu kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyama vingine.

Pia, katika siku ya upigaji kura, vyama vya siasa, wagombea, wanachama au wafuasi wao kukodi au kutumia usafiri wa aina yoyote kubeba wapiga kura kwa madhumuni ya kuwashawishi kumpigia mgombea kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!