Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vurugu za wafugaji, wakulima zafukuta Kongwa
Habari za Siasa

Vurugu za wafugaji, wakulima zafukuta Kongwa

Wakinamama na watoto kutoka wilaya ya Kongwa, wakiwa nje ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa lengo la kufikisha malalamiko yao
Spread the love

WAKULIMA zaidi ya 70 wakiwemo watoto, wanafunzi pamoja na wanawake wamefanya maandamano ya amani kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili wamuelezee kilio chao cha kuporwa maeneo yao ya kilimo. Anaripoti Danson Kaijage, Kongwa … (endelea).

Wakulima hao wakiongozwa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Nalau kijiji cha Kiteto, kata ya Lenjulu, Daimon Chimulu alisema kuwa wakulima hao wamelazimika kufanya maandamano kutoka wilayani Kongwa na kuja jijini Dodoma kuonana na Waziri Mkuu ili kuweza kumuelezea kero zake za kuporwa mashamba yao ya Lumilumi na kutaka maeneo hayo yatumiwe na wafugaji.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti huyo alisema kuwa pamoja na kufanya maandamano kwa ajili ya kuonana na waziri Mkuu ili aweze kutatua mgogoro walionao wa ardhi kati ya wakulima na wafugaji na serikali ya kijiji, juhudi zao za kuonana na Waziri Mkuu zimegonga mwamba kutokna ana Waziri Mkuu kutokuwepo ofisini wala nyumbani kwake kwa kuelezwa kuwa yupo kwenye ziara za kikazi.

Mwenyekiti huyo alisema kilio chao wakulima hao ni kutaka kupewa mashamba yao ili waweze kuendelea na shughuli zao za kilimo kwani kwa sasa hawajui hatima ya maisha yao licha ya kuwa wapo katika maeneo hayo kwa muda mrefu na tayari wameifa fikisha malalamiko hayo kwenye ngazi mbalimbali za uongozi lakini hakuna ufumbuzi.

“Sisi wakulima wa eneo la Lumilumi tunahitaji kujua hatia yetu kwani tumezuiliwa kufanya shughuli zetu za uzalishaji kwa maana ya kilimo na tumeambiwa tusifanynye shughuli yoyote ya kilimo wala wafugaji wasiingize mifugo katika maeneo hayo.

“Jambo la kushangaza kwa sasa tumekuwa tukiona mifugo ikiingia katika maeneo yetu na kula mazao yetu,jambo ambalo lisasababisha kuwepo kwa viashiria vya machafuko au kutoweka kwa amani kutokana na mgogoro huo imefikia hatua ya wafugaji sasa kuanza kuwashambulia wakulima kwa fimbo huku hakuna hatua yoyote ya kisheria ikichukuliwa” alisema Mwenyekiti wa wa kitongoji cha Nalau.

Akizungumzia adha hiyo alisema kuwa kwa sasa wakulima wanakumbana na adha kubwa ya kukosa eneo la kulima ikiwa ni pamoja na kupambana na wafugaji jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko ambayo yanweza kusababisha kuwepo kwa machafuko na kuodosha amani kati ya wakulima na wafugaji.

Kwa upande wa Diwani wa wa kata hiyo Sembuli Chilongola (CCM) alisema kuwa ni kweli yapo malalamiko ya wakulima kwa kutaka wapatiwe maeneo ya kulima lakini kinachozuia ni kutokana na vikao mbalimbali vilivyofanyika na kuwepo kwa makubaliano ya pamoja kuwa eneo linalogombaniwa liwe ni malisho .

Diwani huyo alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wakulima ni wakati sasa wa wakulima kutisha tena mkutano kwa leongo la kuomba kupewa eneo la kuendesha shughuli za kilimo tofauti na ilivyo sasa kwani hata wakulima hao wakienda kwa Waziri Mkuu hakuna hatakayeweza kubadilisha maamuzi ya matumizi bora ya ardhi kama yalivyotengwa.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi alisema kuwa mgogoro huo unafahamika na tume ilisha undwa kwa ajili ya kufuatilia ngogoro huo ambao watu watatu walitoka kwa wakulima na watu watatu walitoka kwa wafugaji na mwenyekiti wa tume hiyo alikuwa Afisa ardhi wa Wilaya ya Kongwa.

Alisema kuwa baada ya kuundwa kwa tume hiyo ya ushuruhisho ilibainika kuwa yapo maeneo ya malisho yalisha ingiliwa na kutokana na hali hiyo ilitolewa amri kwa maeneo hayo yasitumike kwa wakulima wala wafugaji hadi hapo itakapopatikana suluhu.

“Lakini wakulima wenyewe walitaka kuungilia eneo la Lumilumi ambalo limeziuliwa wakati maeneo mengine ya pembezoni yaliruhusiwa,lakini wakati wa msimu wa kilimo mwaka jana wakulima walianza kuingiza matrekta jambo ambalo halikuwa sahihi.

“Lakini kimsingi bado kuna changamaoto kubwa hasa kwa wakuima wakati wa kutoa haki ukitoa haki kwa wafugaji wakulima wanaanza kusema kuwa umepewa rushwa na usipotoa haki na wao wnazidi kusongea katika maeneo hayo, changamoto kubwa ni kutofuatwa kwa sheria ya ardhi Na.5 ya mwaka  1999 toleo la mwaka 2002 ambapo kijiji mwisho wake ni kutoa heka 50, lakini unakuta vijiji vimetoa heka zaidi ya 50 hadi 200 na kupelekea maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya malisho kuwa mashamba,” alisema Ndejembi.

Naye mchungaji wa kanisa la Tanzania Missionary Revival (TMRC) Dikson Chulei ambaye aliwapokea waandamanaji hao alisema kuwa viongozi waote wawe wa Kiroho au kiserikali wanatakiwa kutenda haki kwa wali waliopo chini yao.

Mchungaji Chulei alisema kuwa yeye amewapokea waandamanaji hao na kuwapatia sehemu ya kulala na kuwapatia chakula kwani yeye kama mtumishi wa Mungu pamoja na washirika wake wametimiza wajibu wao wa kuwasaidia watu ambao ni wahitaji.

Alisema kuwa ifahamike kuwa kila mtu anatakiwa kupata haki yake na kama wakulima hao wanastahili kupatiwa haki ni bora wapatiwe haki kwani si vyema kutoa maamuzi ya kupendeleo kwa wale wenye kuwa na kipato kikubwa huku wenye kipato kidogo wakiwa wanatelekezwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!