Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vurugu mkutano wa Waitara, Meya  jiji la Mwanza alazwa rumande
Habari za Siasa

Vurugu mkutano wa Waitara, Meya  jiji la Mwanza alazwa rumande

James Bwire, Meya wa Jiji la Mwanza
Spread the love

POLISI Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania, limemkamata na kumhoji, Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire kwa tuhuma zinazomkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Bwire ambaye ni Diwani wa Mahina kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), anatuhumiwa kuandaa kikundi cha watu, waliovuruga mkutano wa Naibu Waziri wa Tamisemi, Mwita Waitara alioufanya katika moja ya kata za Jiji hilo tarehe 27 Mei, 2020.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro akizungumza na waandishi leo Jumamosi tarehe 30 Mei, 2020 amesema, walimkamata jana jioni Meya Bwire na kumhoji kwa saa 4 kisha wakamalaza rumande.

“Baada ya kuwa hapatikana kwa urahisi, askari polisi ambao moja ya jukumu lao kumfuata na akaletwa jana jioni kwa mahojiano kulingana na tuhuma nzito ambazo sisi tulizipata.”

Mwita Waitara, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI

“Ni kweli alishikiriwa na kwamba tarehe 27 Mei 2020, Naibu waziri wa Tamisemi (Mwita) alifanya kikao katika moja ya Kata jiji la Mwanza na zikapatikana taarifa meya wa jiji hili, aliandaa kikundi cha watu ambacho kikao kinafanyika, kilifanya fujo, kikatoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi ya waziri na Serikali na kusababisha kuvunjika kwa kikao kile,” amesema

Amesema, kutokana na tuhuma zito, walimhoji kwa saa nne na kutokana na mazingira, alipumzishwa na kuendelea tena kwa mahojiano hadi alipomaliza leo na kuachiwa kwa dhamana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!