Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vituko ofisi ya Meya Dar
Habari za Siasa

Vituko ofisi ya Meya Dar

Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam
Spread the love

WAKATI Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akipewa siku 14 kukabidhi ofisi hiyo, Ofisi ya Halmashauri ya Jiji sasa imeamua kumweka nje ya ofisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Isaya amefika ofisini kwake leo tarehe 13 Januari 2020, ili kuendelea na majukumu yake ya kawaida ya kila siku, lakini amekuta nywila (password) ya mlango wa kuingia ofisini kwake imebadilishwa.

Kituko hicho kinachofanywa na Halmashauri ya Jiji, kimelenga kumzuia Meya Isaya kuingia ofisini ili kuendelea na majukumu yake.

Dhamira ya Sipora Liana, Mkurugenzi wa Jiji hilo imeendelea kudhihiri nguvu yake kwa kushirikiana na Abdallah Chaurembo, Meya wa Temeke.

Taarifa ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zinaeleza, msingi wa msukumo unaofanywa na Liana na Chaurembo, unatokana na msimamo wa Meya Isaya kugoma kuelekeza fedha za wananchi katika miradi isiyo na tija.

“Hata Makonda (Pauli Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) haelewi kwa undani kilicho nyuma ya pazia. makonda anaungana na wenzake kwa kuwa tu ni CCM lakini hajui kiini cha mvutano huu.

“Miongozi mwetu hatupendezwi na hili, kinachotukwanza ni kwa kuwa linasimami wan a mkurugenzi na Chaurembo. Kwa mujibu wa taratibu Isaya bado meya,” ameeleza mjumbe mmoja wa CCM aliyeshiriki kikao kilichoshindwa kumng’oa Meya Isaya kutokana na kutokamilika akidi.

Jana tarehe 12 Januari 2020, Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Jiji alisema, “kinachoongeza msukumo wa yote haya ni muwasho wa kutumia fedha za umma na kuzielekeza kwenye miradi isiyo na tija jambo ambalo Meya Mwita hakubaliani nalo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!