Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa vijiji wasakwa na Jeshi la Polisi, kisa bangi
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa vijiji wasakwa na Jeshi la Polisi, kisa bangi

Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Arusha linawasaka viongozi wa kijiji cha Kisimiri Juu kilichopo wilayani Arumeru kwa tuhuma za kukiuka agizo la serikali pamoja na kukwamisha msako wa bhangi kijijini hapo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hayo yalisemwa jana tarehe 27 Septemba 2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng’azi wakati kizungumza na Wanahabari mkoani humo.

Kamanda Ng’azi alisema kuwa, viongozi hao walifunga ofisi huku wanakijiji wakijificha wakati wa msako uliofanyika alfajiri ya jana baada ya Jeshi la Polisi kudokezwa kuhusu usafirishaji wa bangi uliopangwa kufanyika jana.

“Tunaendelea kuwatafuta viongozi wa kamati za ulinzi na usalama na wa kijiji, kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria kwa kuwa wana wajibu wa kuhakikisha katika eneo lao hakuna biashara ya dawa za kulevya inayofanyika.

“Viongozi hao wamekiuka agizo la serikali linalomtaka kila kiongozi katika eneo lake ahakikishe kwamba halilimwi bhangi,” alisema Kamanda Ng’azi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!