Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa dini waonywa
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa dini waonywa

Spread the love

BAADHI ya viongozi wa Dini ambao wamekuwa wakiwaaminisha na kuwataka waumini wao kupokea Baraka zitokanazo na miujiza ya Mungu bila kufanya kazi wameonywa na kusema kuwa kwa kufanya hivyo ni sawa na mtu kumjengea Imani ya Uzezeta na utahila. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …(endelea)

Onyo hilo limetolewa hivi karibuni na askofu wa Jimbo la Dodona na Nyanda za Juu Kusini, Kanisa la Mlima wa Moto, Jijini Dodoma, Silvanus Komba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kufundisha waumini wao somo juu ya kufanya kazi kwa bidii na Maarifa.

Askofu Komba alisema kuwa kwa sasa viongozi wengi wamekuwa chanzo cha kuwafanya waumini kuwa masikini kwa kutokana na kushindwa kuwafundisha jinsi ya kufanya kazi kwa bidii na badala yake wanaaminishwa zaidi katika kupokea miujiza.

Askofu Komba alisema kuwa pamoja na kuwa anaamini kuwa miujiza ipo lakini ni wajibu wa kila muunini kufanya kazi zake kwa bidii ili uweze kupata muujiza kupitia kwenye kazi husika inayofanyika badala ya kujibweteka bila kufanya kazi na kusubiria miujiza.

Alisema hakuna mtu ambaye anaweza kupata mafanikio kama hataweza kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwani kufanya kazi ni mpango kamili wa Mungu na siyo mapenzi ya mwanadamu kama watu wanavyofikiria.

“Napenda kusema kuwa Bidii ya Mtu ndiyo utajiri wake kila my afanye kazi kwa bidii na kwa maarifa na bila kuchagua kazi ili aweze kujiingizia kipato yeye, familia na taifa kwa ujumla wake na huko ndiko unakoweza kukutana na muujiza wa mafanikio.

“Hata maandiko matakatifu yanaeleza kuwa “Tengeneza kazi yako” yakimaanisha kuwa boresha au fanya kazi kwa bidii ili uweze kuelekea katika mafanikio, lakini hauwezi kushinda ndani umelala na ukadhani kuwa utapata Baraka au utajiri.

“Sisi viongozi tusiwadanganye watu kwa kuwaaminisha katika mafanikio yanayotokana na miujiza licha ya kuwa miujiza ipo lakini ni jambo jema kuwafundisha waumini kupata mafanikio kutokana na kufanya kazi kwa bidii na maarifa zaidi” alisema Askofu Komba.

Askofu Komba alisema kuwa anakerwa na tabia ya kuwaminisha waumini kuwa watapokea magari, majumba, kazi na kumiliki vitegauchumi vya nguvu na kwenye maombi waumini wamekuwa wakidakishwa upepe kama ishara za kupokea mafanikio yao.

Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa umefika wakati sasa wa neno la Unabii ni watu kufanya kazi kwa bidii na maarifa badala ya kusubiri miujiza na kuongeza kuwa mtu yoyote ambaye hafanyi kazi anamkosea Mungu kwani maagizo ya Mungu ni kufanya kazi kwa bidii.

“Tusiwafundishe watu utaila, mimi nimeisha waambia waumini wangu na baadhi ya viongozi ndani ya kanisa kila mmoja anapaswa kufanya kazi na bila kudharau kazi,kila mtu afanye kazi ambayo ni halali, mwenye kuuza nyanya, mchicha,kahawa, kulima na kila aina ya kazi ni lazima afanye na afanye kwa bidii na maarifa.

“Nimeanza na wachungaji wangu kila mchungaji ni lazima anioneshe kazi anayofanya tofauti nay a utumishi kwani kazi ya utumishi ina muda wa kuifanya na siyo saa zote nataka kujua saa ambazo haufanyi kazi ya Mungu unafanya kazi gani.

“Kama nilivyosema ninaanza na wachungaji, mashemasi,wazee wa kanisa na viongozi wote wa Idara sambamba na kutaka kila mshirika aoneshe mradi au kazi ambayo anaifanya kwa lengo la kumuongezee kipato na siyo kukaa kanisani anasubiri Muujiza, utapata muujiza bila kufanya kazi hilo jambo halipo kabisa” alisema Askofu Komba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!