Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa dini waombwa kuombea uchaguzi mkuu 2020
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa dini waombwa kuombea uchaguzi mkuu 2020

Askofu wa Kanisa la Power of God lililopo eneo la Chanika, Dankon Rwaikila
Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Power of God lililopo eneo la Chanika, Dankon Rwaikila amewaomba watumishi wa dini kumuomba Mungu ili atuchagulie viongozi wenye hofu ya Mungu watakaoweza kujitoa katika nchi yetu ambao wataleta maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza hayo jana Jumapili tarehe 28 Juni 2020 wakati wa ibada maalumu kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari ambapo shule zimefunguliwa leo Jumatatu.

Rwaikila amesema watumishi hao wa dini watakapokuwa na mshikamano wa kumuomba Mungu taifa litapata viongozi wazalendo ambao wenye hofu ya Mungu watakaoweza kujitoa katika nchi yetu.

Pia, maombi hayo yatasaidia kupata viongozi ambao wataweza kuunga juhudi za Rais John Magufuli watakaoweza kutupeleka kwenye ndoto ya Tanzania mpya.

“Ninachojua, jambo zuri linapotaka kutokea shetani anajiinua, hivyo biblia inasema ukimuomba Mungu atatuepusha na mabaya kwenye nchi yetu atupe mshikamano ili tumalize uchaguzi wetu tukiwa na amani na umoja,”amesema Rwaikila.

Waumini wa Kanisa la Power of Godwakiwa kwenye ibada

Pia, amesema wazazi na walezi waendelee kumwamini Mungu kwa kuwa atawalinda watoto wanapokuwa shuleni na Mungu ataendelea kuliokoa taifa na janga hilo la ugonjwa wa Corona.

Wakati huo huo,  Askofu wa Kanisa la Reviral and Praise Fellowship lililopo Chanika, Edmund Kihwili alisema, Mungu ataendelea kuwalinda wanafunzi shuleni kwa kuwa wengi wanahofu wakijua ugonjwa haujaisha hivyo wazazi wanatakiwa wawapeleke watoto wao shuleni.

“Kinachotakiwa kumuamini Mungu na kumthamini, tumeona ushindi na mkono wa bwana umetenda kwa kutuepusha na ugonjwa huu wa Corona,” amesema Kihwili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!