Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijiji vinne kuondoka gizani kabla ya mwakani
Habari Mchanganyiko

Vijiji vinne kuondoka gizani kabla ya mwakani

Mafundi umeme wakiwa kazini
Spread the love

WANANCHI wa vijiji vinne vya kata ya Ulaya, wilaya ya Kilosa, Morogoro wanatarajia kuondoka gizani kufuatia mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu kuanza ujenzi wake unaotarajia kukamilika Desemba 30 mwaka huu. Anaripoti Christina Haule, Kilosa … (endelea).

Mmoja wa wakati wa kata hiyo, Juma Mohamed alisema wanaimani kukamilika kwa mradi huo kutawasaidia kuondokana na adha ya kukaa gizani nyakati za usiku sambamba na kufanya biashara mbalimbali zitakazowaongezea kipato.

Mohamed alisema adha kubwa waliyokuwa wakiipata ikiwemo kukosa uwezo wa kununua umeme wa sola kwa kutoa sh 1000 kwa siku kwa umeme wa sola ambayo hawana kutokana na uchumi mdogo.

“Nilipo nina umri wa miaka 57 sasa, sijawahi kuona umeme, nampongeza Rais Magufuli (John) sababu ilikuwa ni ndoto kupata umeme,” alisema.

Naye Meneja wa Tanesco wilaya ya Kilosa, Daniel Makalla alisema lengo ni kuhakikisha ikifika mwaka 2021 vijiji vyote, vitongoji na Taasisi wilayani humo na kila mtu atakuwa na huduma ya umeme na kwamba itafikia mahali mtu anamaliza kujenga na kuweka umeme.

Alisema uwepo wa umeme utasaidia jamii ikiwemo vijana kuweza kunufaika kwa kufungua shughuli ndogo ndogo za ujasiliamali ikiwemo kuchomelea, kuranda mbao na saloon za kike na za kiume.

Awali Ofisa kutoka Tanesco Morogoro, Hussein Kachambwa aliwataka wananchi wilayani humo kulinda miundombinu hiyo na kuwa makini na vishoka kwa kufuata utaratibu wa kuchukua fomu wenyewe pale wanapotaka umeme kwenye nyumba zao.

“Kuna watu wanatapeliwa badala ya Sh. 27,000 atakwambia lete laki nne hapa ya haraka haraka nikusaidie, tukifuata utaratibu wenyewe wa kwenda kuchukua fomu itatusaidia kuepukana na vishoka,” alisema.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ulaya, Erasto Matokeo alisema umeme huo utasaidia kukuza uchumi wa wanakilosa kutokana na hali halisi ya kata ilikuwa nyuma kimaendeleo kutokana na kukosa umeme ambapo kwa sasa wanaweza kupata viwanda vikubwa na vidogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!