Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko VIGUTA wawaliza wananchi
Habari Mchanganyiko

VIGUTA wawaliza wananchi

Spread the love

WAKAZI zaidi ya 300 katika Mkoa wa Dodoma wametapeliwa na Umoja wa Vikundi vya Vikoba Tanzania (VIGUTA) kwa kuwachangisha fedha kwa nia ya kuwajengea nyumba na kuuza viwanja  kwa bei nafuu bila mafanikio. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wananchi hao walisema kuwa kitendo cha VIGUTA kuwakwamisha wananchi kwa maendeleo na kushindwa kutimiza malengo yao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Endeshi Raideison alisema kuwa kitendo cha VIGUTA  kushindwa kuteleleza kile walichokihaidi ni kuwakwamisha wananchi maendeleo yao.

Endeshi alisema kuwa wananchi wengi wamejikuta wakihangaika kutafuta fedha pamoja na kukopa benki kwa ajili ya kulipia asilimia kumi kwa lengo la kujengewa nyumba kwa lengo la kupata kwa bei nafuu jambo ambalo halikukamilika.

Kwa upande wake, Diwani wa viti maalum kata ya Loje, Wilaya ya Chamwino, Hilda Kadunda akizungumza na waandishi wa habari juu ya sakata hilo, ambaye pia alikuwa Meneja wa VIGUTA Wilaya ya Chamwino aliyekuwa akiwawakilisha wananchi, alisema kuwa wananchi wengi wamedhurumiwa na VIGUTA jambo ambalo limesababisha usumbufu mkubwa.

Diwani huyo alisema awali VIGUTA waliwashawishi wananchi kuwa watawajengea wananchi kwa bei nafuu na ikiwa na kuwauzia viwanja watakuwa wakilipa asilimia kumi kulingana na gharama ya nyumba na baadaye kuendelea kulipa kidogo kidogo.

Akizungumzia juu ya Chamwino, Hilda alisema kuwa baada ya viongozi wakuu wa VIGUTA kukimbia na fedha za watu imekuwa tatizo kubwa ambalo linasababusha wasimamizi waliopo kuonekana ni matapeli.

“Mimi nimekuwa msimamizi katika wilaya ya Chamwimo na tumefanikiwa kujenga nyumba kwa mujibu makubaliano yaliyotakiwa, tumejenga nyumba ya serikali ya mtaa, pamoja na nyumba nyingine ambazo zimefikia hatua ya mikanda lakini huduma hiyo imesitishwa.

“Wapo wananchi ambao waliingiza pesa zao benki kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na kupewa viwanja lakini zoezi hilo hikufanyika kutokana na hali hiyo wananchi wamecharuka na kutaka walipwe fedha zao.

“Mimi kama msimamizi wa VIGUTA niliyekuwa nasimamia Chamwino na kuwahamasisha wananchi kujiunga katika makundi ili kupata unafuu lakini baada ya zoezi kutokamilika nilipelekwa mahakamani na kuonekana kama tapeli.

“Nikapelekwa mahakamani ila namshukuru Mungu nilishinda kesi na kuomba mahakama inipe kibali cha kuuza nyumba ya serikali ya mtaa ambayo imejengwa na Viguta kama ya mfano ili niweze kuwalipa wale wanaodai kutokana na jengo hilo kutokuwa limelipwa na serikali ya kijiji,” alisema Hilda.

Kutokana na hali hiyo Hilda alisema kuwa anaiomba serikali kuwakamata viongozi wakuu wa VIGUTA ili waweze kuwalipa wananchi fedha zao badala ya kuwaachilia kuendelea na mambo yao huku wananchi wakiendelea kusumbua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!