RAIS wa Tanzania, John Magufuli leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020 analihutubia Bunge la 11 na kulivunja jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea),
Bunge hilo la 11 linaloongozwa na Spika Job Ndugai lilizinduliwa na Rais Magufuli tarehe 20 Novemba 2015.
Tayari wageni mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa wamekwisha kuwasili ukumbini kumsubiri Rais Magufuli kuingia ndani ya ukumbi huo.
Baadhi ya wageni hao ni; Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.
Pia, Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Mohamed Ali Shein, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Makamu wa Rais mstaafu wa Tanzania, Mohamed Gharib Bilal.
Kulifunga Bunge hilo, kunatoa fursa ya mchakato wa uchaguzi mkuuutakaofanyika Oktoba 2020 kuanza.
Wengine waliopo ni, mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye, Mizengo Pinda na Edward Lowassa.
Pia, Spika Mstaafu Anne Makinda, Jaji Mkuu mstaafu, Othuman Chande, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni miongoni mwa waliojitokeza katika shughuli hiyo ya kihistoria.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi
Leave a comment