Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na viongozi wengine wakiwasili mahakamani

Vigogo hawa kutikisa Kisutu leo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo inatarajia kusikiliza kesi ya vigogo tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti  Faki Sosi … (endelea).

Miongoni mwa vigogo hao ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa; Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Viongozi hao wa Chadema wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya mikisanyiko isiyoruhusiwa, kuhamasisha chuki, kushawishi watu kutoridhika na hata kula njama.

Viongozi hoa wanatarajiwa kuendelea na utaratibu wa kimahakama kwa kila mmoja kukabiliana na mashitaka yake.

Kumekuwepo na mahudhurio makubwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwenye kesi ya kisiasa inayomuhusisha Mbowe na Matiko.

Mbowe na Matiko walifikishwa mahakamani tarehe 23 Novemba 2018 kwa madai ya makosa kadhaa ikiwemo kufanya mkusanyiko usioruhusiwa na baadaye kukataliwa dhamana.

Kesi zingine zinazotarajiwa kusikilizwa leo ni pamoja na ya wafanyabiashara Seth Harbinder na James Rugemarila pia waliokuwa viongozi wa Timu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey na Nyange.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo inatarajia kusikiliza kesi ya vigogo tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti  Faki Sosi ... (endelea). Miongoni mwa vigogo hao ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa; Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, John Heche, Mbunge wa Tarime vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini. Viongozi hao wa Chadema wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya mikisanyiko isiyoruhusiwa, kuhamasisha chuki, kushawishi watu kutoridhika na hata kula njama. Viongozi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram