Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vifo vya ‘Mwamposa’: Kanisa labebeshwa gharama
Habari Mchanganyiko

Vifo vya ‘Mwamposa’: Kanisa labebeshwa gharama

Spread the love

SERIKALI imesema, Kanisa la Inuka Uangaze la Mchungaji Boniface Mwamposa, lina jukumu la kugharamia msiba wa watu 20 waliofariki wakati wa kukanyaga mafuta ya upako. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Na kwamba, taratibu za awali zinafanywa na serikali lakini suala la majeneza, kusafirisha watu na ndugu zao waliofika kwenye kanisa hilo, zinatakiwa kubebwa na kanisa lenyewe.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 3 Februari 2020 na Anna Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambapo amesema, wamekuwa wakiwasiliana na kiongozi mkuu wa kanisa hilo aliyeko Kenya ili kubeba jukumu hilo.

“Kwa kweli wao ndio wanaotakiwa kugharamia majeneza, usafiri wa kuwapeleka marehemu kwao pamoja na ndugu zao waliokuja kuwachukua,” amesema Mghwira.

Kiongozi wa kanisa hilo aliyemtaja kwa jina moja la Maboya na kwamba, amekuwa akimtafuta tangu jana bila mafanikio, lakini sasa tayari amepata namba yake rasmi na amemtumia ujumbe.

Amesema, ibada ya kuaga maiti hao imeanza leo saa tano asubuhi huku taratubu za awali zikiendelea kufanyika.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Februari Mosi, 2020 baada ya kongamano la kidini ambapo waumini hao walikuwa wakigombea kukanyaga mafuta ya upako, yaliyomwagwa kwenye mageti ya uwanja wa Majengo.

Kibali cha kingamano hilo la siku tatu, kiliombwa na Elia Mwambapa, Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God na kwamba, mchungaji huyo aliomba mafuta hayo kutoka kwa Mchungaji Boniface Mwamposa.

Mpaka sasa Mchungaji Mwambapa na Mwamposa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na tukio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!