MAREKANI imeendelea kuwa taifa linaloongoza kwa vifo vinavyotokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Kwa mujibu wa mtandao wa Worldmeter unaonyesha, hadi leo Jumamosi tarehe 16, 2020 saa 6:00 mchana, Marekani ilikuwa imeripoti maambukizo milioni 1.4, vifo 88,507 huku waliopona wakiwa 327,751.
Mtandao huo unaonyesha, maambukizi duniani yamefikia milioni 4,641,975, vifo 308,827 huku waliopona milioni 1,768,005.
Hispania ni taifa linalofuatia baada ya Marekani likiwa na maambukizi 274,367, waliopona 188,967 huku vifo vikiwa 27,459.
Urusi inashika nafasi ya tatu duniani ikiwa na maambukizi 272,043, vifo 2,537 na waliopona ni, 63,166.
Leave a comment