Uwanja wa Taifa sasa kuitwa, Uwanja wa Mkapa

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amebadili jina la uliokuwa Uwanja wa Taifa na sasa kuwa unaitwa Uwanja wa Mkapa katika kumuenzi Hayati Mkapa kwenye mchango wake kwenye sekta ya Michezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Uwanja huo ambao ulianza kujengwa mwaka 2003 chini ya utawala wa Hayati Benjamini William Mkapa baada ya kuahidi kujenga Uwanja huo mwaka 2000 na kukamilika mwaka 2007.

Magufuli amefanya maamuzi hayo mapema leo alipokuwa anahutubia Taifa wakati wa tukio la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Hayati Mkapa, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kusema kuwa marehemu hakupenda vitu vingi viitwe kwa jina lake.

“Mzee Mkapa atakumbukwa kwa mchango wake kwenye michezo kwa kujenga Uwanja mkubwa wa Taifa na watu wengi wamependekeza uwanja huo uitwe jina lake kwa ajili ya kumuenzi, licha ya yeye mwenye hakupenda vitu vingi viitwe kwa jina lake.

Rais John Magufuli akishindwa kujiuza machozi kumtoa

“Basi kwa sababu hiyo kuanzia leo Uwanja huo utaitwa Mkapa katika njia ya kamuenzi,” alisema Rais Magufuli.

Uwanja huo, ulikamilka mwaka 2007 chini ya utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete katika serikali ya awamu ya nne, wenye uwezo wa kubeba watazamaji 60,000 ulioghalimu dora za kimarekani 56 milioni.

Uwanja huo unashika namba 12 kwa ukubwa barani Afrika kwa sasa na kuchezwa michezo mikubwa ya kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu ya Taifa.

Mkapa aliyefariki usiku wa tarehe 23 Julai mwaka huu, baada ya kuugua kwa muda mfupi, anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwake Lupaso mkoani Lindi.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amebadili jina la uliokuwa Uwanja wa Taifa na sasa kuwa unaitwa Uwanja wa Mkapa katika kumuenzi Hayati Mkapa kwenye mchango wake kwenye sekta ya Michezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea) Uwanja huo ambao ulianza kujengwa mwaka 2003 chini ya utawala wa Hayati Benjamini William Mkapa baada ya kuahidi kujenga Uwanja huo mwaka 2000 na kukamilika mwaka 2007. Magufuli amefanya maamuzi hayo mapema leo alipokuwa anahutubia Taifa wakati wa tukio la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Hayati Mkapa, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Kelvin Mwaipungu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!