Rais John Magufuli alipokuwa anaomba kura

UVCCM wamkera Rais Magufuli kwa rushwa

LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kujipambanua kuwa kinapambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, bado baadhi ya  jumuiya ndani ya chama hicho ziimeonekana kukumbwa na kashifa ya rushwa na ufisadi wa kutisha, anaandika Dany Tibason.

Hali hiyo ya baadhi ya jumuiya kukumbwa na kashifa ya rushwa, imeooneekana kumtisha na kumkera mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli.

Akifungua Mkutano wa tisa wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ambao pia unaambatana na uchaguzi wa viongozi kwa ngazi ya taifa Rais Magufuli amesema amesikitishwa na kuwepo kwa vitendo vya kwa baadhi ya viongozi ndani ya jumuiya hiyo.

Muda mfupi wakati akifungua mkutano huo Rais Magufuli amesema licha ya chama hicho kupambana na rushwa na ufisadi lakini mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa…. pamoja na mjumbe mmoja wapo sero kwa tuhuma za kutoa na kupokeea rushwa kwa ajili ya kununua uongozi.

Mwenyekiti wa CCCM Taifa amesema ni jambo la aibu kwa vijana wa CCM kukumbwa ba kashifa la rushwa na kuwaelekeza vijana kutowapatia nafasi vijana ambao wanaonekana kutuhumiwa kwa kutoa au kupokea rushwa.

Amesema kijana ambaye ana kashfa ya rushwa hasipatiwe nafasi yoyote ndani ya uongozi wa vijana kwa maana hawawezi kuwa watenda kazi wema ndani ya jumuiya hiyo.

Mbali na Rais Magufuli kukerwa na vitendo vya rushwa pia ametangaza kuifuta bodi ya UVCCM kwa maelezo kuwa haina msaada wowote kwa jumuiya hiyo.

Amesema vijana wana miradi mingi lakini bado kuna wajanja wachache ambao wamekuwa wakijichotea hela kwa ajili ya kujinufaisha badala ya vijana kunufaika.

LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kujipambanua kuwa kinapambana na vitendo vya rushwa na ufisadi, bado baadhi ya  jumuiya ndani ya chama hicho ziimeonekana kukumbwa na kashifa ya rushwa na ufisadi wa kutisha, anaandika Dany Tibason. Hali hiyo ya baadhi ya jumuiya kukumbwa na kashifa ya rushwa, imeooneekana kumtisha na kumkera mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli. Akifungua Mkutano wa tisa wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ambao pia unaambatana na uchaguzi wa viongozi kwa ngazi ya taifa Rais Magufuli amesema amesikitishwa na kuwepo kwa vitendo vya kwa baadhi ya viongozi ndani ya jumuiya hiyo. Muda…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube