Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uungu’ wa Msajili wa Vyama kuanza na Lissu, Zitto  
Habari za SiasaTangulizi

Uungu’ wa Msajili wa Vyama kuanza na Lissu, Zitto  

Spread the love

NGUVU za kimamlaka zilizowekwa kwenye sheria ya vyama vya siasa na kupigiwa chapuo na baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), zaweza kutumika kuwashughulikia baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa upinzani na hata wale wa kutoka chama tawala. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa wahenga wa kwanza wa sheria hiyo, ni Tundu Lissu, mbunge wa Chadema katika jimbo la Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa chama hicho; Zitto Zuberi Kabwe, mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo; Nape Nnauye, mbunge wa Mtama (CCM) na Hussen Bashe, mbunge wa Nzega (CCM).

Hakuna shaka kuwa Zitto, Lissu, Nape na Bashe na wengine wanaofanana nao, wakiwamo watetezi wa haki za binadamu, wanatajwa kuwa watakuwa waathirika wa kwanza wa “sheria hiyo kandamizi.”

Kabla ya kupitishwa kwa muswada huo bungeni mjini Dodoma jana, tarehe 29 Januari 2019, kuliibuka msuguano mkubwa na waziwazi kati ya baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa upinzani.

Pamoja na vifungu vingine vigumu vilivyomo kwenye sheria hiyo, tishio kubwa la kidemokrasia, kifungu cha 21E ndio kinaweza kutumika kuzima sauti za wakosoaji wakubwa wa serikali.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, msajili anaweza kusimamisha ushiriki wa mwanachama yoyote wa chama chochote cha siasa kufanya kazi za siasa kwa maana ya kumwondoa kwenye ulingo huo.

Maisha ya kisiasa ya Lissu, Zitto, Nape, Bashe na wengine wanaofanana na wengine wanaoikosoa serikali, yanaweza kuishia njiani kupitia kifungu hicho.

Msajili wa vyama vya siasa, ni mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala.

Lissu, Zitto, Bashe na Nape, wamekuwa mwiba kwa serikali ya Rais Magufuli; tangu kiongozi huyo aingie madarakani Novemba 2015, kumetungwa sheria nyingi kandamizi.

Kwa sasa, Lissu yuko nchini Ubelgiji anakotibiwa majeraha ya risasi yaliyotokana na shambulio lililofanywa nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na wanaoitwa “watu wasiojuliika.”

Mara kadhaa, Lissu na Zitto, wamefunguliwa mashtaka kadhaa mahakamani, huku Nape akiondolewa kwenye uwaziri katika mazingira ya kutatanisha na kisha kutishiwa kwa bastora.

Aidha, Zitto na Lissu, wamekumbana na adhabu kadhaa bungeni kutokana na matamshi yao dhidi ya serikali ama Bunge lenyewe. Maisha yao ya kisiasa yanaweza kuwa mabaya sana katika kipindi hiki.

Sakata la kuzuiwa ndege aina ya Bomberdier Q 400-Dash 8 nchini Canada, ni miongoni mwa mambo ambayo Lissu aliyasimamia na kuibua mjadala mpana nchini.

Bomberdier Q 400-Dash 8 iliyonunuliwa na serikali nchini Canada, ilikamatwa na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd, kufuatia amri ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro (ICSD). Amri hiyo ilitolewa mwaka 2010 na ilitaka serikali kulipa kampuni hiyo dola za Marekani 38 milioni (sawa na Sh. 87 bilioni).

Lissu amekuwa na kauli ngumu jambo ambalo linasababisha kuonekana mwanasiasa tofauti kidogo, miaka mitatu iliyopita aliibuka na kauli ya “Dikteta Uchwara,” jambo ambalo lilimsababishia kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la uchochezi.

Pamoja na matukio mengine ya huko nyuma na kuwa nje ya nchi, Lissu ameendelea kusigana na serikali kutokana na kuzungumzia mwenendo wa serikali ya awamu ya tano huku serikali nayo ikimjibu.

Akiwa huko huko Ubelgiji, Lissu amekwaruza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kumtaka arejee nyumbani na kuendelea na wajibu wake wa kibunge, yeye (Lissu) anasema bado yu mgonjwa, hata hivyo katika Bunge hili Ndugai anaweza kuamua lolote juu ya ubunge wa Lissu.

Zitto naye amekuwa mwenyeji kwenye mahakama mbalimbali nchi, akikosekana mwezi huu basi mwzi ujao anaweza kushtakiwa akiwa Dar es Salaa ama popote ndani ya miapaka ya nchi hii.

Zitto huyu ndiye aliyeibuka na sakata la TSh. 1.5 trilioni ambazo hazikuonekana matumizi yake katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2016/17.

Sakata la Sh. 1.5 trilioni liliibua serikali ambapo katika nyakati tofauti walitoa matamko ya kupinga madai hayo na kwenda mbali zaidi kwa kutoa ufafanuzi kuhusu mahali zilipo fedha hizo ikiwemo kutumika katika hati fungani.

Hoja hiyo ya Zitto bado haijapatiwa majibu na katika Bunge hilo na mpaka sasa, serikali imeshindwa kujieleza vizuri juu ya suala hilo. Zitto anaendelea kusota mahakamani akituhumiwa kwa makosa matatu ya uchochezi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!