Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Utata: Uhamiaji wamkana Kabendera
Habari Mchanganyiko

Utata: Uhamiaji wamkana Kabendera

Spread the love

IDARA ya uhamiaji nchini, imekana kuwahi kumuhoji mwandishi wa habari za uchunguzi ndani na nje ya Tanzania, Erick Kabendera kuhusu uraia wake. Anaripoti Mwandihi Wetu … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 31 Julai 2019 jijini Dar es Salaam, Gerald Kihinga, Kamishna wa Uraia na Pasipoti kutoka Idara ya Uhamiaji amekana kwamba Kabendera hakuwahi kuhojiwa na Uhamiaji.

Kumbukumbu mbalimbali ikiwemo vyambo vya habari, zinaonesha kuwa Kabendera aliwahi kukutana na dhahama hiyo mwaka 2013.

Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyoripoti mahojiano kati ya Kabendera na Uhamiaji ni gazeti la The Citizen la tarehe 13 Mei 2013. Mwisho wa mahojiano hayo viliripoti kuwa ‘hakuna utata.’

Dk. Emannuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani aliunda kamati iliyofanya kazi ya kuchunguza uraia wa Kabendera.

Kwa mujibu wa kumbukumbu hizo, Dk. Nchimbi aliwaagiza maofisa wa uhamiaji kutowasumbua wazazi wa Kabendera kuhusiana na uraia wao, ni baada ya Kabendera kuandika barua ya malalamiko kuhusu kusumbuliwa.

Leo tarehe 31 Julai 2019 ikiwa ni miaka takribani sita, idara ya uhamiaji inarejea kufanya kile kile ilichokifanya mwaka 2013 cha kuhoji uraia wa Kabendera huku ikikana kuwahi kufanya hivyo.

Kihinga amesema, idara hiyo ilimkamata Kabendera baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu utata wa uraia wake.

Na kwamba, ni kutokana na mwanahabari huyo kukaidi wito wa kufika katika ofisi za idara hiyo kwa ajili ya mahojiano kuhusu suala hilo.

“idara ya uhamiaji ni chombo kilichopewa mamlaka ya kuchunguza uraia wa mtu yeyote anayetiliwa mashaka, ikiwa tumepokea taarifa kutoka kwa mtu yeyote. Jukumu la utambuzi wa uraia linafanywa bila kujali dini, rangi na wadhifa wa mtu katika jamii,” amesema Kihinga na kuongeza:

“Bwana Kabendera alikuwa hajawahi kuhojiwa kuhusiana na uraia wake, kwa kuwa hakufika ofisi za uhamiaji pamoja na kutumiwa wito wa kuitwa mara nyingi lakini hakuweza kufika katika ofisi za uhamiaji.”

Kihinga ameeleza kuwa, kwa sasa Kabendera anahojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusu suala hilo.

“Hivyo basi, idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi iliweza kumtafuta na kumpata mpaka tunapoongeza hivi, bwana kabendera tunaye sisi na tunaendelea kumuhoji kuhusu utata wa uraia wake.”

Aidha, Kihinga amekanusha taarifa za utata wa tukio la kukamatwa kwa Kabendera akisema, ni kutokana na muhusika kushindwa kutoa ushirikiano wa Idara ya Uhamiaji.

“Ielelweke kwamba uchunguzi wa utata wa uraia imekuwa ikifanyika kwa watu mbalimbali ikiwemo watu mashughuli, hivyo suala hili limekuwa kubwa sana kwa sababu huyu bwana ni mwandishi wa habari,” amesema Kihinga.

“…lakini tumekuwa tukiwahoji watu wengi, vitu hivi haviko wazi sababu hawakukimbia, walitoa ushirikiano,  wakiambiwa walete vitu analeta tofauti na Kabendera.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

error: Content is protected !!