January 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uswizi yaeleza wasiwasi juu ya mawakala wa haki za Watibeti

Spread the love

KRYSTYNA Marty, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali Uswizi amefanya mazungumzo na Qin Gang, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuhusu mahusiano ya kiuchumi, haki za kibinadamu China na hali ya janga la COVID-19. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea). 

Wakati wa mazungumzo hayo, Uswizi ambaye ni mshirika wa tatu mkubwa wa China kibiaahara, alieleza wasiwasi wake juu ya “kutokuheshimiwa kwa haki za binadamu nchini China” hususan namna mamlaka za China zinavyowatendea watu wa jimbo la Tibeti.

Hii inakuja kufuatia ziara ya Balozi wa Uswizi, Bernardino Regazzoni nchini China Septemba 2020, katika Jimbo la Tibeti ambayo ni ziara ya kwanza rasmi kwa Uswizi tangu mwaka 2017.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ushirikiano wa Mambo ya Nje ya Uswizi katika ziara hiyo ilisema, kuwa Balozi wa Uswizi pamoja na wanadiplomasia 10, walitembelea miji ya Lhasa na Shigatse na kutumia nafasi hiyo kuzungumza na Serikali za Mitaa za miji hiyo juu ya mambo muhimu ikiwemo suala la haki za binadamu.

Aidha, kuhusu mahusiano ya kibiashara, tayari Uswizi ambaye ni mshirika wa tatu mkubwa kibiashara wa China, amewekaza kiasi cha pesa ya Uswisi (CHF) bilioni 36.

Uswizi pia imesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiahara, uwekezaji na fedha za miradi katika nchi zinazoendelea, sambamba na mpango wa mradi wa Ukanda wa Kiuchumi na Barabara mwaka 2019.

Hata hivyo, mwaka 2019 China iliahirisha mazungumzo na Uswizi juu ya Haki za Binadamu baada ya Uswizi na nchi zingine 21, kusaini barua kwenda Umoja wa Mataifa (UN) kukosoa uwepo wa kambi za mateso huko Mashariki mwa Turkestan.

error: Content is protected !!