Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Ushoga’ wa Bulaya, Mdee, wazua mjadala mahakamani
Habari za Siasa

‘Ushoga’ wa Bulaya, Mdee, wazua mjadala mahakamani

Spread the love

JESTER Amos Bulaya, mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), amedai mahakamani kuwa uhusiano wake na mbunge mwenzake wa Kawe, Halima James Mdee, “unafungwa na ujirani” wao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, “mimi na Halima Mdee, ni marafiki wa kawaida kabisa. Urafiki wetu, unatokana na kuwa tunaishi majirani, huko Mbweni, jijini Dar es Salaam.”

Bulaya amelazimika kueleza hayo, kufuatia upande wa mashitaka, ukiongozwa na wakili mkuu mwandamizi wa serikali, Simoni Wankyo, kuiambia mahakama kuwa Bulaya amekuwa na uhusiano na Mdee, kiasi kilichosababisha hadi kuvunja ndoa yake.

“Siyo kweli kwamba ndoa yangu imevunjika na imevunjwa na urafiki wangu na Mdee. Bado ninaishi na mume wangu, aitwaye Gustavu Babile, katika eneo la Mbweni na kwamba Mdee, ni jirani yetu,” ameeleza Bulaya.

Katika swali lake la awali, Wankyo alimtaka Bulaya kuithibitishia mahakama iliyokuwa chini ya Hakimu Mkuu Mkazi, Thomas Simba, kwamba ni sahihi kuwa ndoa yake na Babile, ilivunjika?

Bulaya alisema, alifunga ndoa ya kanisani na mume wake huyo mwaka 2003 na kwamba ndoa ya Kanisani haivunjiki. 

Hata hivyo, wakati Bulaya anaeleza kuwa yeye na mume wake wanaishi nyumba moja humo Mbweni,  kuna taarifa kuwa Bulaya anaishi pamoja na  Mdee, Dodoma na Dar es es Salaam na kwamba wawili hao, wanatumia gari moja.

Bulaya ni mshitakiwa wa tisa katika kesi hiyo ya uchochezi inayomkabili mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na viongozi wenzake wengine, akiwamo Bulaya.

Wengine waliomo kwenye kesi hiyo, ni mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa; katibu mkuu wa Chadema na mbunge wa Kibamba, John Mnyika; aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko. 

Washitakiwa wote wanakabiliwa na mashitaka 13, likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa Februari 1 na 16 mwaka 2018, jijini Dar es Salaam, walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.

Aidha, washitakiwa wote wanadaiwa kuwa 16 Februari 2018, katika barabara ya Kawawa, maeneo ya Kinondoni Mkwajuni, wakiwa na wenzao ambao hawapo mahakamani, walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la afisa wa Polisi, mwenye cheo cha SSP, Gerald Ngiichi, kwa kugoma kutawanyika na kusababisha uvunjifu wa amani. 

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, hatua ya viongozi hao wa Chadema, kugomea kutekeleza maelezo ya Polisi, kulipeĺekea kuwapo kwa hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline, pamoja na majeruha kwa askari wawili ambao ni  H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.

Akizungumzia utata uliyoibuka kwenye hati yake ya kusafiria, ambako inadaiwa kuwa awali Bulaya alieleza mahakama kuwa siku ya tukio hili alikuwa safarini nchini Afrika Kusini.

Akihojiwa na wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, kuhusu utata wa maelezo yake yaliyomo kwenye hati yake ya kusafirià, Bulaya alisema: “Hakuna màhali popote palipogongwa mhuri pakionesha nilisafiri nje ya nchi kati ya Februari 16 hadi 28 mwaka 2018.”

Amedai kuwa alichoieleza mahakama, ni kwamba Februari 16 mwaka 2018, aliwahi kuondoka katika mkutàno wa kufunga kampeni kwa kuwa “rafiki yake Mdee,” alikuwa anaumwa hivyo walienda kujiandaa na safari ya kwenda kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni, ulifanyika katika viwanja vya Buibui, Mwananyamala.

Bulaya amesema, hajawahi kuieleza mahakama kuwa siku waliyosafiri na katika hati yake ya kusafiria imegongwa mhuri katika ukurasa wa 17.

Katika hatua nyingine, Bulaya amekiri kuwa  hakuna sheria inayoruhusu chama cha siasa, kuhamasisha wafuasi wake, kudai haki kwa maandamano ama vurugu.

Baada ya kueleza hayo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 20 hadi 24 mwakani àmbapo shahidi wa 10 wa upande wa utetezi, anataràjiwa kutoa ushahidi wake. 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!