Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ushirikina; Binti akutwa uvunguni mwa bibi yake hajitambui
Habari za Siasa

Ushirikina; Binti akutwa uvunguni mwa bibi yake hajitambui

Spread the love

TUKIO la Mwanafunzi wa Shuele ya Sekondari Ikinabushu (jina limehifadhiwa) kukutwa chini ya uvungu wa kitanda cha bibi yake, limetikisa viunga vya mji wa Bariadi, Simiyu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa zaidi zinaripoti kwamba, mwanafunzi huo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu tarehe 25 Januari mwaka huu hapo kijijini kwao Ikinabushu na baada ya siku tano alikutwa chumbani kwa bibi yake akiwa hajitambui.

Binti huo inaeleza kwamba, alikuwa akiishi kwenye nyumba aliyokuwa akiishi bibi yake (Kwandu Kiuluma) na ndugu zake wengine akiwemo mama yake wa kambo na ndugu zake.

Kaka wa binti huo Samson Lambo amesema kuwa, aliambiwa na baba yake mdogo anayeishi Kigoma kwamba, amepokea taarifa za kupotea kwa mdogo wake na kwamba, yeye hakua akijua kuhusu ndugu mkasa huo.

Samson anasema, alipoanza kufuatilia na kuuliza, baadhi ya watu walimweleza kwamba, walikutana na mdogo wake huyo kwenye ghala maeneo ya nyumbani kwao na walipomwita alikataa na kuingia kwenye ghala hilo.

“Nilipopata taarifa hizo niliongeza wasiwasi kuhusu kupotea kwake. Kama familia tulikaa na kuamua kumtafuta kwa njia mbadala ili kujua alipo,” amesema Samson na kuongeza;

“Kwenye kikao chetu cha familia baada ya kuamini kuna mambo ya nguvu za giza, tulikubaliana kumwita mganga. Baada ya mganga kufanya dawa zake, akatuambia kuwa mtoto yupo ndani.”

Samsoni anasema, walimuuliza mganga huyo kwamba humo ndani anapatikana wapi?, ndipo walipoambiwa wakamwangalie chini ya uvungu wa kitanda cha bibi yake na kumkuta akiwa amelala hapo.

“Tulichofanya ni kumtoa kwani alikuwa na madaftari yake ya shule na alituomba maji na chakula,” amesema.

Mwanafunzi huo alisema kuwa, hana kumbukumbu yoyote kama alitoweka lakini siku moja akiwa kitandani, aliwaona watu wengi wanaume kwa wanawake wamemzunguka akiwemo bibi yake huyo.

Binti huyo amesema kuwa, alikuwa akienda shule kama kawaida na anashangaa kuambiwa kwamba hakuwa akienda shule, “mimi nashangaa kuwa eti siendi shule, najiona nilikuwa naenda shule kila siku.”

Hata hivyo, bibi huo (Kwandu) licha ya kukiri binti huyo kukutwa chini ya uvubgu wa kitanda chake, alisema hahusiki na kuongeza;

“Labda kuna watu wamefanya hivyo kupitia mimi lakini sihusiki kwa kupotea kwa mjukuu wangu.”

Deusdedit Nsimeki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ameeleza kuwa, wanamshikilia bibi huo kwa mahojiano zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!