Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Urais Z’bar: Maalim Seif amtumia salamu Dk. Mwinyi

Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, amemtumia salamu Dk. Hussein Mwinyi, Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Maalim Seif ametuma salamu hizo leo Jumatano tarehe 5 Agosti 2020, saa kadhaa baada ya kuteuliwa na Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo kuipeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo.

Mwenyekiti huyo wa ACT-Wazalendo amemtaka Dk. Mwinyi ajiandae na uchaguzi huo huku akiahidi kushirikiana naye vizuri kama Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, endapo atashinda katika uchaguzi huo.

“Nitume salamu kwa watawala, zama za kubambikizia Wazanzibar watawala wasio na ridhaa zao zimekwisha, Maalim Seif wa mwaka 2020 ni Maalim wa ACT-Wazalendo tutaongoza Wazanzibar kushinda na kulinda ushindi wao,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amesema “Nimwambie ndugu yangu Dk. Mwinyi ajiandae dhidi ya Maalim Seif, mimi na yeye tutafanya kazi vizuri sana chini ya Seriakli ya Umoja wa Kitaifa.”

            Soma zaidi:-

Wakati huo huo, Maalim Seif ametaja mambo kumi atakayoyafanyia kazi atakapochaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 27 na 28 Oktoba 2020.

Baadhi ya mambo hayo ni, kurejesha utii wa Katiba na utawala wa sheria, wakati la pili ikiwa ni kujenga utengamano wa umoja wa kitaifa na maridhiano.

Maalim Seif ameahidi kuimarisha heshima na haki ya Wazanzibar katika Muungano, wakati la nne ikiwa ni kuimarisha misingi ya haki za binadamu.

“Nitasimamia ujenzi wa uchumi imara itakayobadilisha sura ya Zanzibar ndani ya muda mfupi na kuwa mfano wa kuigwa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Nitafanya Zanzibar kuwa kituo kikuu cha biashara na fedha,” amesema Maalim Seifa ambaye tangu mwkaa 1995 amekuwa akigombea urais kupitia CUF na mwaka huu atakuwa ACT-Wazalendo,

Maalim Seif amesema, atakalotekeleza ni kuboresha huduma za afya, kwa kujenga hospitali zenye vifaa tiba bora pamoja na watumishi wa kutosha.

Dk. Hussein Mwinyi, Mgomnbea Urais Zanzibar (CCM)

“Nitasimamia maslahi ya makundi maalum wakiwemo wanawake, watoto, wazee waathirika dawa za kulevya na ukimwi,” amesema Maalim Seif

Mgombea huyo Urais wa Zanzibar wa ACT-Wazalendo, amesema atahakikisha inairudishia Zanzibar uanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (CAF).

About Masalu Erasto

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!