Felix Tshisekedi

Upinzani washinda uchaguzi DRC, Kabila chali

MGOMBEA wa upinzani, Felix Tshisekedi wa Chama cha UDPS ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), tume ya uchaguzi imesema. Vinaripoti vyombo vya kimataifa….(endelea).

Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na “anatangazwa mshindi wa urais mteule.”

Tshisekedi alipata zaidi ya kura milioni saba 7 huku Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni na mgombea anayeungwa mkono na serikali, Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.

Tayari tume ya uchaguzi imemtangaza mpinzani kushinda uchaguzi huo.

MGOMBEA wa upinzani, Felix Tshisekedi wa Chama cha UDPS ameshinda uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), tume ya uchaguzi imesema. Vinaripoti vyombo vya kimataifa....(endelea). Matokeo ya awali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali Emmanuel Shadary. Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi wa urais mteule." Tshisekedi alipata zaidi ya kura milioni saba 7 huku Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni na mgombea anayeungwa mkono na…

Review Overview

User Rating: 1.8 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram