Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Upatu, utakatishaji fedha wawapandisha kortini
Habari Mchanganyiko

Upatu, utakatishaji fedha wawapandisha kortini

Spread the love

MAGDALENA Uhwello na Halima Nsubuga leo tarehe 21 Agosti 2019, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka saba likiwemo ya utakatishaji fedha. Anaripoti Regina Mkonda … (endelea).

Mashitaka hayo yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Shitaka la kwanza; Wanatuhumiwa kula njama katika kusimamia na kuendesha shughuli za upatu, wakidaiwa kwamba walitekeleza kosa hilo katika tarehe tofauti mwaka 2017 wakiwa jijini Dar es Salaam.

Shitaka la pili; watuhumiwa hao wanadaiwa  kati ya tarehe 1 Aprili 2017 na Juni 30 2017, walisimamia shughuli za upatu kinyume cha sheria na kukusanya fedha kutoka kwa watu wakiwaahidi kupokea faida kutokana na fedha zao.

Katika shitaka la tatu; Watuhumiwa hao walisomewa kosa la utakatishaji fedha haramu wakidaiwa kwamba, kwenye nyakati tofauti mwaka 2017 wakiwa jijini Dar es Salaam, waliingiza Dola za Marekani 394,265 kwenye akaunti namba 3004211400319 kwa jina la Magdalena na Halima.

Fedha hizo ziliingizwa katika Benki ya Equity ya nchini Tanzania huku wakijua, pesa hizo ni mazalia ya kuendesha shughuli haramu za upatu kinyume cha sheria.

Shitaka la nne; Ni utakatishaji fedha wa kiasi cha Dola za Marekani 12,309 katika akaunti 1002100721913 ya Equity Benki ya Uganda yenye jina la Smart Protus Magara zilizotokana na shughuli za upatu.

Shitaka la tano; Ni utakatishaji fedha wa kiasi cha Dola za Marekani 29,086 wanazodaiwa kuziingiza katika akaunti 1002100721913 ya Equity Benki ya Uganda yenye jina la Smart Protus Magara.

Kwenye shitaka la sita; Watuhumiwa hao wanadaiwa kuficha chanzo cha fedha kiasi chaDola za Marekani 58,743 zilizoingizwa kwenye akaunti namba 1002100721913 ya Equity Benki ya Uganda yenye jina la Smart Protus Magara zilizotokana na shughuli hiyo.

Shitaka la saba; Ni utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Marekani 83718 walizoingiza katika akaunti namba  1002100721913 ya Equity Benki Uganda yenye jina la Smart Protus Magara.

Washitakiwa wote wamekana mashtaka hayo. Baada ya kuwasomea mashtaka washitakiwa hao, Wakili Wankyo amesema, upelelezi wa shauri hiyo haujakamilika lakini uko katika hatua za mwisho na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe kusikilizwa.

Hakimu Simba amewanyima dhamana washitakiwa kwa kuwa, mashtaka yao hayana dhamana. Hakimu Simba amepanga kesi hiyo ya jinai namba 167 ya mwaka 2019 kusikilizwa tarehe 30 Agosti 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!