Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Upasuaji wa sehemu za siri za kike waongezeka
AfyaRipoti

Upasuaji wa sehemu za siri za kike waongezeka

Spread the love

NI jambo la kawaida kufanya marekebisho ya kitabibu katika viungo vya mwili wa binadamu kama vile  makalio, nyonga, ngozi na sura. Hata hivyo, hivi karibuni, huko Uingreza, kumekuwa na urekebishaji wa sehemu za siri hasa za wanawake, anaandika Mwandishi wetu.

Wanawake wengi hasa wenye umri ulio chini ya miaka 20 wamekuwa wanatembelea hospitali kutafuta huduma hiyo ambapo mpaka kati ya mwaka 2015 na 2016 wasichana wapatao 200 wamefanya marekebisho hayo.

Madaktari wa Uingereza wanathibitisha hilo na kusema kwamba, wasichana wa miaka 11 hadi 13 ambao wanafikiria uke wao unatatizo kwamba labda una umbo lisilo sahihi, ni mnene au mdogo sana na wanakerwa nao.

Kuna sababu nyingi za kurekebisha sehemu za siri za mwanamke.  Zote zinahusiana na anatomia ya mwanamke. Kwa kuangalia tokea nje, katika hali ya kawaida, uke unayo midomo minene, yaani midomo miwili ya nje (labia major) na midomo miwili ya ndani (labia minor), ambapo mara nyingi, midomo ya ndani huwa imefunikwa na midomo ya nje.

Lakini, kwa baadhi ya wasichana midomo miwili ya ndani inakuwa ni mikubwa kuliko midomo miwili ya nje. Katika hali hii, mwanamke huweza kupata maumivu wakati wa kuendesha baiskeli, kufanya mazoezi, au wakati wa kufanya tendo la ngono.

Hivyo, wasichana wengi wanaomba kufanyiwa upasuaji huo ili kupunguza midomo ya uke, kuimairisha kujiamini miongoni mwa wanawake wakati wa tendo la ngono, kuongeza kujiamini wakati wakufanya mazoezi ya viungo, na kuwa na mwonekano wa kuvutia katika sehemu zao za siri.

Katika upasuaji huo, ambao kwa Kiingereza unaitwa “labiaplasty,” daktari huweza kupunguza urefu wa midomo miwili ya ndani ya uke.

Wakati mwingine,  daktari hupunguza urefu wa govi la kisimi (clitoral hood), pale ambapo govi hilo linaleta matatizo kama ya midomo miwili ya ndani ya uke iliyorefuka kupita kiasi.

Tukiangalia katka jamii zetu za kiafrika suala hilo la urekebishaji wa sehemu za siri za mwanamke ni sawa  na baadhi vitendo vya ukeketaji vinavyopingwa na jamii.

Kimsingi, kuna aina tatu za ukeketa wa wanawake. Katika aina ya kwanza (clitoridectomy), kisima au kisimi pamoja na govi lake hukatwa.

Katika aina ya pili (excision), kisima na midomo ya ndani ya uke hukatwa, lakini bila kuigusa midomo ya nje.

Katika aina ya tatu (infibulation),  midomo ya ndani na midomo ya nje ya uke hukatwa na kisha kuungansihwa ili kupunguza kipenyo cha uke, lakini bila kukikata kisimi.

Kwa ujumla, ukeketaji unayo madhara mengi. Madhara hayo  hayo ni pamoja na kupungua kwa hamu ya tendo la ngono,  kupatwa na maumivu mkali wakati wa kujifungua na kutokwa na damu nyingi wakati huo.

Hivyo, mtazamo wa madaktari ni kwamba panahitajika elimu  na uhamasishaji wa kutosha kuhusu sehemu za siri za mwanamke na inafaa kutolewa kwa wasichana wakiwa bado wadogo ili kuwaeleza kuwa kuna tofauti katika maumbile ya uke wa mwanamke na mwingine kama ilivyo kwa nyuso zao. Na hivyo hakuna sababu ya kuhangaika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!