Upasuaji wa kifua wafanikiwa JKCI

WATOTO tisa wenye umri kuanzia miezi mitatu hadi 17 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Shirika la Chain of Hope la Uingereza kuanzia tarehe 23 hadi 27 Julai, 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo kwa umma na Kitengo cha Uhusiano Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), na kusema kuwa, watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambapo madaktari hao wametengeneza valvu na kuziba matundu.

Pamoja na kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya, kurekebisha mfumo wa uzungukaji wa damu katika moyo na kuweka valvu za bandia kwa wale walio na valvu za moyo zilizoharibika.

“Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na sita kati yao wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

WATOTO tisa wenye umri kuanzia miezi mitatu hadi 17 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Shirika la Chain of Hope la Uingereza kuanzia tarehe 23 hadi 27 Julai, 2018. Anaripoti Regina Kelvin ... (endelea). Taarifa hiyo imetolewa leo kwa umma na Kitengo cha Uhusiano Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), na kusema kuwa, watoto waliofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambapo madaktari hao wametengeneza valvu na kuziba matundu. Pamoja na kurekebisha mishipa ya moyo ambayo imekaa vibaya, kurekebisha…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram