Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uozo sakata la Meya Dar waanikwa
Habari za SiasaTangulizi

Uozo sakata la Meya Dar waanikwa

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

UAMUZI wa madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka kumsimamisha kazi Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita umeibua uozo ndani ya jiji hilo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea). 

Leo tarehe 12 Januari 2019, Saed Kubene, Mbunge wa Jimbo la Ubunge (Chadema) na Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Jiji hilo amesema, hakuna namna ya kumzuia Meya Mwita kufanya shughuli zake, isipokuwa wafanya mambo mawili; kuvunja jiji au kuanza upya mchakato wa kumng’oa.

“Wametuchezea sana, sasa wamefika mwisho. Wakitaka kumng’oa Meya waanze mchakato upya ama wavunje jiji. Vinginevyo, hawawezi kufanya na tutawazuia kufanya chochote,” amesema Kubenea.

Akifafanua kilichotokea kabla na kwenye kikao kilichoitishwa na Sipora Liana, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, kilichofanyika tarehe 10 Januari 2020, Kubenea amesema tuhuma na mchakato uliofanyika ulikiuka kanuni na taratubu za jiji.

Akizungumzia tuhuma za Meya Mwita ambaye ni Diwani wa Vijibweni, Kigamboni (Chadema), Kubenea ametaja baadhi ya tuhuma alizobebeshwa meya huyona kufafanua.

Meya huyo anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya gari la ofisi ambapo Kubenea amesema, mtuhumiwa wa kwanza kwenye hilo sakata alipaswa kuwa mkurugenzi wa jiji ambaye ameshindwa kumsimamia mwajiri wake (dereva).

“Meya haajiri, anayeendesha gari ni mwajiriwa wa jiji. Meya Mwita ni abiria, Trafiki anawezaje kumfungulia kesi abiria badala ya dereva aliyekuwa akiendesha gari?” amehoji Kubenea.

Amesema, kwenye vikao vyote vya jiji, kamati haijawahi kupokea malalamiko yoyote kama Meya wa Jiji anatuhumiwa kuendesha gari vibaya, “shitaka hili ni upuuzi mtupu,” amesema.

Akizungumzia tuhuma kwamba Meya Mwita amezuia kutumia Sh. 5.8 Bil zilizotokana na mauzo ya Hisa za Shiriks la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Kubenea amesema, miongoni mwa wajumbe waliounga mkono kutotumia fedha hizo ni Abdallah Chaurembo, Meya wa Temeke ambaye ndio aliyembebesa Meya Mwita tuhuma hizo.

“Fedha hizi tulikataa zisitumike kwa kuwa, kulikuwa na mambo mengi ya kifisadi, kwanza uuzwaji wa hisa wenyewe ni wa kifisadi na uamuzi wa kutotumia fedha hizo sio wa meya, ni wa jiji.

“Halmashauri walikuja na azimio la kutoka fedha hizo zitumieke kwa ajili ya mradi wa wanafunzi, tukakataa. Tukawaambia mradi kama huo walianzisha UVCCM na walishindwa,” amesema kubenea.

Amefafanua zaidi kwamba mkurugenzi Liana amekua akianzisha miradi kadhaa ili fedha hizo zitumike, lakini jiji lilikataa kutokana na miradi hiyo kutokuwa na tija.

“(Mkurugenzi wa Jiji) akaja na kununua mabasi ya utalii, tukakataa maana hapa Dar es Salaam hakuna utalii wa namna hiyo. Tukasema hakuna upembuzi mzuri wa mradi huo. Tulipopiga kura na Meya alipopiga kura ya kukubaliana kuachana na mradi huo, hapo akaonekana tatizo.

“Wakataka tutoe Sh. Bilioni 3 kupanua Kituo cha Mabasi ya Mikuoani-Ubungo, tukakataa kwa kuwa tayari serikali ilishatoa fedha kujenga akituo cha Mbezi. Yaani huyu mkurugenzi alikuwa anawashwawashwa kutumia fedha hizo,” amesema Kubenea.

Amesema, tuhuma za Meya Mwita kwamba alishindwa kusimamia kikao cha madiwani na kusababisha vurugu hazina maana, na kwamba anayemtuhumu meya ndio aliyesababisha vurugu hizi.

Akimzungumiza Chaurembo, Kubenea amesema hana usafi wa kumnyooshea yeyote kidole katika suala la maadili “mimi ni mwandishi, namjua vizuri Chaurembo, hana usafi huo.”

Amesema, hakuna mazingira yanayohalalisha Meya Mwita kutokuwa Meya wa Jiji na kwamba, hata hatua ya Liana kuweka saini feki ya mjumbe kikao cha kumng’oa meya, kinatosha kikao hicho kupoteza sifa.

“Kama mtu anakiri fojari za mahudhurio jambo la hadharani, anafanya mangapi akiwa sirini?” amehoji Kubenea na kuongeza “akidi ya mbili ya tatu haikutimia, unawezaje kuhalalisha kumwondoa meya?”

Mbunge huyo wa Ubungo amesema, ndani ya kikao cha baraza hilo kilichotumika kupokea ripoti na kupiga kura, Meya Mwita hakupewa nafasi ya kujitete ikiwa ni haki yake ya msingi.

“Si hivyo tu, kamati haikuonesha popote kama Meya Mwita amehojiwa. Haikuonesha kama amekiri makosa ama ameomba msamaha, hakuna. Utetezi wake haukuoneshwa kwenye ripoti hiyo,” amesema.

Amesema, wajimbe hawakuwa tayari kuelekeza fedha za wananchi katika matumizi yasiyoeleweka, huyu ana msimamo wa matumizi ya fedha, “haitawezekana kuendesha kikao chochote asiwepo Meya Mwita. Tunajua kwamba Mwita ni meya halali wa Jiji la Dar es Salaam.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!