Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ummy Mwalimu mgeni rasmi, kampeni ya linda ardhi ya mwanamke
Habari Mchanganyiko

Ummy Mwalimu mgeni rasmi, kampeni ya linda ardhi ya mwanamke

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Linda ardhi ya Mwanamke, itakayofanyika tarehe 21 Novemba, mwaka huu, inayotetea Haki za Ardhi za Mwanamke nchini. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Hayo yalisemwa jana na Mchambuzi wa masuala ya Ardhi kutoka Shirika la kimataifa linalochochea na kuangazia ulinzi wa haki za ardhi za kijinsia kwa waliopo mijini na vijijini – Landesa, Khadija Mrisho wakati wa mafunzo kwa wanahabari kutoka mikoa mbalimbali Tanzania.

Alisema, Tanzania ni nchi ya kwanza kuanza kutekeleza kampeni hiyo, kufuatia kuwepo kwa utashi wa kisiasa na ushirikiano wa Taasisi za kiraia na Serikali kwa ujumla zinazoangalia ni namna gani wanahakikisha haki za mwanamke zinalindwa.

Mrisho alisema, kampeni hiyo inalenga kukusanya nguvu ya pamoja kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ngazi ya kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia, shirika la Global Louching Network na Shirika la Habitat for Humanity, ambao wanaweka nguvu ya pamoja kwenye vitendea kazi, fedha na utaalam wa kusaidia utekeleza wa kampeni kwa ngazi ya nchi.

Alisema kama taasisi, katika kuendeleza kampeni hiyo, wataendelea kutafuta fedha ili kuifanya kampeni kuwa endelevu nchini.

Mrisho alisema, kampeni hiyo ya miaka 12 kuanzia 2019 inaenda sanjari na mpango wa dira ya maendeleo endelevu ya ajenda ya 2030 ambao itatekelezwa kwa awamu kwa miaka mitatu mitatu.

Aidha alisema, kampeni hiyo ilizinduliwa kimataifa kwenye mkutano wa Benki ya Dunia nchini Marekani mwezi Machi 2019 ambapo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kitaifa Novemba 21 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Alisema, kampeni hiyo itatekelezwa nchi nzima kufuatia kusambaa kwa wadau ambao ni taasisi zinazohusika na masuala ya kutafuta haki kwa wanawake kwenye mikoa yote ya Tanzania kufuatia kuainishwa kwa changamoto mbalimbali za ardhi ambazo zinapatikana maeneo mbalimbali ya nchi.

Naye Mwanasheria kutoka Shirika la Landesa, Godfrey Massay amewaasa wanawake kuzingatia na kuzitumia sheria zilizopo ili kuweza kupata haki zao kufuatia sheria zilizopo kutambua haki ya mwanamke.

Alisema sheria namba 4 -5 ya mwaka 1999 ya ardhi za vijiji inatambua umiliki wa ardhi wa kati ya mwanamke mwenyewe na mwanaume kwa pamoja.

Alisema, katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zina sheria nzuri za masuala ya usimamizi wa ardhi na kutambua haki za mwanamke.

Massay alisema, sheria hizo zimepewa jina la mapinduzi ya mfumo dume na kwamba zina vifungu vizuri ambavyo vikitekelezwa vinavyoweza kuondoa changamoto ya haki za mwanamke.

Alisema changamoto iliyopo ni utekelezaji wa sheria hizo zilizopo na kwamba kuna haja ya kufanya jambo ili sheria hizo zitekelezwe vizuri kwa maslahi ya wanawake.

Naye Mkurugenzi wa zamani na Muasisi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Edda Sanga alisema upo umuhimu wa waandishi wa habari kupewa nafasi ya kuinua kampeni hiyo kufuatia kutumia muda wa miaka zaidi ya 9 kusemea masuala ya haki za mwanamke katika kumiliki ardhi na kuitumia kiuchumi.

Sanga ambaye pia ni  mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya Landesa alisema, Tanzania inapozungumzia masuala ya kukua kwa viwanda na uchumi wa kati haiwezekani kwa namna yoyote kuwasahau wanawake lakini utafiti unaonesha ni asilimia 24 tu ya wanawake ndio wanamiliki ardhi huku nyingine ikitumiwa na wanaume kwa kiwango kikubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!