Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Ummy aingilia kati Mwalimu kumpiga mwanafunzi mpaka kufa
Elimu

Ummy aingilia kati Mwalimu kumpiga mwanafunzi mpaka kufa

Waziri wa Nchi Ofisi a Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Ummy Mwalimu
Spread the love

TUKIO la Mwalimu Respecious Patrick wa Shule ya Msingi Kibeta, iliyoko Bukoba mkoani Kagera anayedaiwa kumwadhibu mwanafuzi  Sperius Eradius, na kupelekea mwanafunzi huyo kufariki dunia, limemuibua Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Tume ya Utumishi wa Walimu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Waziri Ummy amemwagiza mtaalamu bingwa wa uchunguzi kwenda mkoani Kagera kwa ajili ya kurejea uchunguzi wa chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo na kuwahakikishia wanafamilia na wananchi kuwa uchunguzi utafanyika kwa ufanisi na haki itatendeka.  

Waziri Ummy amesema kuwa kitendo hicho ni cha ukatili kwani ni kinyume na Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 kifungu cha 13 (2) ambayo inasisitiza kutolewa kwa adhabu stahiki kwa mtoto kulingana na umri, hali ya kimwili na kiakili.

Aidha, amelaani vikali tukio hilo na kusema kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa uchunguzi, anaamini pindi uchunguzi utakapokamilika hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.

Naye Katibu Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu Winifrida Rutaindurwa, amemuagiza  Kaimu Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Bukoba kufuatilia kuhusu tukio hilo na kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu na. 25 ya mwaka 2015 pindi itakapobainika masuala yanayohitaji kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa walimu wa shule hiyo, sheria ichukue mkondo wake.

Rutaindurwa ametoa agizo hilo leo tarehe 30 Agosti 2018.

“Kwanza nimejiuliza, hadi huyu mwalimu anafikia huko kuna uwezekano mkubwa amekuwa na tabia ya kuwaadhibu wanafunzi kupita kiasi na alipaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu huko nyuma kabla ya kusababisha madhara makubwa hivi,” amesema na kuongeza.

“Nimeshindwa kuelewa inawezekanaje mwalimu anafanya tukio la kumpiga mwanafunzi kiasi hicho na walimu wengine wapo na hakuna jitihada wanazofanya kumsaidia mwanafunzi.”

Katika hatua nyingine, ametoa onyo kwa walimu wanaowaadhibu wanafunzi bila kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu zinazotoa mwongozo wa aina, kiwango na namna  adhabu inavyotakiwa kutolewa kwa wanafunzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!