Mafundi umeme wakiwa kazini

Umeme kukatika Dar es Salaam

Spread the love

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limetangaza katizo la umeme katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilala na Temeke, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa tangazo hilo, katizo hilo litatokea kesho tarehe 22 Oktoba 2019, kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi 10:30 jioni, kwenye njia ya Msongo wa 132KV ili kuruhusu kazi ya kuungwa kebo ya Transfoma mpya.

Tangazo hilo limeeleza kuwa, Transfoma hiyo mpya ina uwezo mkubwa wa Megawati 300MVA, ambayo itasaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme kwa Jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na Pwani.

Maeneo yatakayokumbwa na katizo hilo ni pamoja na, Buguruni, Vingunguti, Tazara, Gongo la Mboto, Ukonga, Mombasa, Mzambarauni, Pugu.

Maeneo mengine ni Yombo, Kitunda, Machimbo, Mwanagati, Mbondole pamoja na baadhi ya maeneo ya Tabata.

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limetangaza katizo la umeme katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Ilala na Temeke, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). Kwa mujibu wa tangazo hilo, katizo hilo litatokea kesho tarehe 22 Oktoba 2019, kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi 10:30 jioni, kwenye njia ya Msongo wa 132KV ili kuruhusu kazi ya kuungwa kebo ya Transfoma mpya. Tangazo hilo limeeleza kuwa, Transfoma hiyo mpya ina uwezo mkubwa wa Megawati 300MVA, ambayo itasaidia kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme kwa Jiji la Dar es Salaam, Zanzibar na Pwani. Maeneo yatakayokumbwa na katizo hilo ni pamoja na, Buguruni,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!