February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Umakamu wa Rais: Je, ni Maalim Seif?

Spread the love

BARAZA la Uongozi la Chama cha ACT-Wazalendo, tayari limependekeza jina la Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), lakini halijataja jina hilo hadharani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). 

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema, Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo kwa mujibu wa Katiba yake, kilifanya kazi yake ya kupendekeza jina na baadaye kwenda kwenye baraza la uongozi kwa ajili ya kupelekwa serikalini.

Ametoa malezo hayo leo tarehe 6 Desema 2020, baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari kama chama hicho kimeishapendekeza jina la Makamu wa Kwanza wa Rais.

“…upendekezaji wa jina la mwanachama ni madaraka ya uongozi wa chama chetu, Kamati Kuu imeishaketi kujadili na kutoa jina moja la mwanachama atakayeshika nafasi ya umakamu wa rais,” amesema bila kutaja jina hilo.

Hata hivyo, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa chama hicho na aliyekuwa mgombea urais visiwani humo, aliwahi kuulizwa na waandishi wa habari kama akakuwa tayari endapo kama atapendekezwa kushika nafasi ya Umakamu wa Rais wa Zanzibar.

Alisema, hajui na chama ndio kitaamua kama nani awe Makamu wa Rais na hapo ndio itajulikana.

Maalim Seif alikuwahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Dk. Ali Mohammed Shein (2010-2015), baada ya maridhiano yaliyoingizwa kwenye Katiba mwaka 2009.

Hata hivyo, baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Dk. Shein aliunda serikali yake bila kuhusisha upinzani kutokana na sintofahamu iliyojitokeza ambapo Chama cha Wananchi (CUF), kilichopata zaidi ya asilimia 10 kususia matokeo hayo.

Bado inadhaniwa, kwamba jina lililopendekezwa, laweza kuwa la Maalim Seif ambaye ni nguli wa siasa za upinzani visiwani humo.

error: Content is protected !!