Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uma, puliza uandikishaji serikali za mitaa
Habari za Siasa

Uma, puliza uandikishaji serikali za mitaa

Spread the love

UANDIKISHAJI wa daftari la wapiga kura kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 24 Novemba 2019, umegubikwa na mitazamo mbalimba. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakishutumu maandalizi hafifu na kusababisha kukosekana msisimko, huku wengine wakidai wamesukumwa na utendaji wa Rais John Magufuli.

Paulo John, Mkazi wa MwembeYanga, Temeke jijini Dar es Salaam amesema, hana mpango wa kujiandikisha na au kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kwa kile alichoeleza kwamba ni kukosa imani na uendeshwaji wa zoezi hilo.

“Mimi sikujiandikisha na sina mpango wa kujiandikisha. Nimesikia mara kwa mara malalamiko ya upinzani, viongozi walishasema hata kama mpinzani akipita, tatizo nani atamtangaza? Kwa hiyo itakuwa sawa na kazi bure,” amesema Paul na kuongeza;

“Nitapoteza muda wangu, sababu nitamchagua mpinzani na hatotangazwa. Na sijaona marekebisho yoyote ya kunishawishi kama mpinzani atapita.

“Tunataka uchaguzi wa huru, kuona kauli za mabadiliko kwamba walikosea kutamka kauli ile. Na watuhakikishie kama kutakuwa na uwazi, lakini bila hivyo tutasumbuana, itakuwa kiini macho.”

Mzee Kasunzu Razalo, Mkazi wa Tandika amesema amejiandikisha katika Orodha ya Wapiga Kura, kwa sababu ya kutii amri ya serikali, na si kwa hiari yake.

“Mimi nimejiandikisha, lakini kujiandikisha kwangu kama unavyoelea katika mfumo tulio nao leo. Unapotetereka kidogo wanakushughulikia, wanaweza kusema asiye jiandikisha atakuwa namna hii, na aliejiandikisha atakuwa namna hii.

Kwa hiyo tunajiandikisha ilimradi tu, lakini mfumo unaoenda wa vyama vingi sio wenyewe,” amesema Mzee Kasunzu.

Wakati baadhi wakilalamika kutoridhishwa na hali ya kisiasa ilivyo, wengine wamesema wanasita kujiandikisha kwa hofu kwamba, watakaowachagua huenda wakawasaliti kwa kujiuzulu na kuhamia katika vyama vingine, kitendo walichokifanainsha na kurubuniwa.

Mustafa Hamad, Mfanyabaishara wa Soko la Stereo Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam amesema kitendo cha baadhi ya wabunge na madiwani kujiuzulu nafasi zao na kisha kugombea tena kimemvunja moyo.

“Tumeona mbunge aliyehama akahamia upande wa pili, yaani ninyi mnaonekana mnapumbazwa fulani. Kwa sababu kuunga juhudi za mheshimiwa, kwa nini usiunge wakati unafanya kazi? Sisi tumemchagua, tumeacha shughuli zetu, siku mbiIi tatu unaambiwa kaacha amemuunga mkono mheshimiwa,

Mbona sisi tunamuunga mkono mheshimiwa kila anachotuambia tunafanya, inaonekana kama kurubunian. Na hata huyu mwenyekiti wa serikali za mitaa tunaye mchagua tunahofia huenda ikawa kama yale yale,” amesema Hamadi.

Wakati huo huo, baachi ya wananchi wamesema wamejiandikisha na watashiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kutokana na kuridhishwa na kasi ya utendaji wa Rais Magufuli.

Juma Mfangavu, Mkazi wa Mbagala amesema mejiandikisha, na atapiga kura kutokana na kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.

“Nimejiandikisha katika kituo cha Bondeni City, ni lazima nipige kura. Napiga kulingana na nilivyopendezwa na serikali iliyopo, na tayari nimeshaona kiongozi atakaye nifaa ni yupi. Atakayeweza kwenda na kasi ya mheshimiwa,” amesema Mfangavu.

Mariamu Ramadhani, Mkazi wa Sinza Uzuri Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kilichomhamasisha kujiandikisha ni kutokana na kuridhishwa na misimamo ya Rais Magufuli, katika kurejesha nidhamu kwenye taasisi za umma, na kupelekea wananchi wa kawaida kuheshimika.

“Kama awamu hii watumishi wamenyooka, naamini nikichagua viongozi wenye msimamo huo nchi itanyooka zaidi,” amesema Mariamu.

Msafiri Aminiel, Mkazi wa Tandika amesema “mimi nimejiandikisha, lazima kura nipige, kwa sababu mpaka nimeenda kujiandikisha ni lazima kura nipige, ningekuwa sitaki kupiga kura nisingejiandikisha.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!