‘Ukivunja ahadi ya ndoa kifungo miaka 10’ – MwanaHALISI Online

‘Ukivunja ahadi ya ndoa kifungo miaka 10’

POLISI nchini India wamemkamata mwanamume mmoja raia wa Scotland kwa madai ya ubakaji baada ya kuvunja ahadi ya ndoa na mwanamke aliyeshiriki ngono naye. Chanzo BBC.

Mwanamume huyo atakabiliwa na kifungo cha miaka 10 gerezani iwapo mahakama nchini humo itamkuta na hatia hiyo.

Mtu huyo alituhumiwa kwa kosa hilo baada ya aliyekuwa mpenzi wake kumshataki kuwa, amevunja ahadi ya kufunga ndoa.

Mwanamme huyo alikuwa akifanya kazi kwenye ukumbi wa mazoezi mjini Delhi na inaarifiwa kuwa alikuwa katika uhusiano na mwanadada huyo kwa muda wa miezi mitano.

Baada ya mwanamme huyo kuvunja uhusiano kati yao, mwanadada huyo aliamua kumshitaki. Anasema kwamba alikubali kufanya naye ngono kwa ahadi ya kufunga naye ndoa.

India iko katika njia panda kuhusiana na mabadiliko ya maadili na mtazamo dhidi ya kushiriki mapenzi nje ya ndoa.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na kesi kadha zinazokabiliana na kuvunjwa kwa ahadi ya ndoa na kuibua swali iwapo ni kosa la ubakaji ukishiriki ngono na mwanamke kisha uvunje ahadi ya kumuoa.

POLISI nchini India wamemkamata mwanamume mmoja raia wa Scotland kwa madai ya ubakaji baada ya kuvunja ahadi ya ndoa na mwanamke aliyeshiriki ngono naye. Chanzo BBC. Mwanamume huyo atakabiliwa na kifungo cha miaka 10 gerezani iwapo mahakama nchini humo itamkuta na hatia hiyo. Mtu huyo alituhumiwa kwa kosa hilo baada ya aliyekuwa mpenzi wake kumshataki kuwa, amevunja ahadi ya kufunga ndoa. Mwanamme huyo alikuwa akifanya kazi kwenye ukumbi wa mazoezi mjini Delhi na inaarifiwa kuwa alikuwa katika uhusiano na mwanadada huyo kwa muda wa miezi mitano. Baada ya mwanamme huyo kuvunja uhusiano kati yao, mwanadada huyo aliamua kumshitaki. Anasema kwamba…

Review Overview

User Rating: Be the first one !
0

About Masalu Erasto

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube