Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ukistaajabu ya Lipumba utayaoona ya Mtatiro
Habari za SiasaTangulizi

Ukistaajabu ya Lipumba utayaoona ya Mtatiro

Spread the love

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amekula matapishi yake baada ya kutangaza kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Matatiro leo Agosti 11, 2018 ametangaza uamuzi wa kujivua uanachama wa CUF na kuonesha nia ya kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kupata fursa ya kuifanyia nchi maendeleo, akidai kwamba ndani ya CUF aliikosa fursa hiyo.

Mtatiro aliyeibuka leo ni yule aliyesema kuwa Lipumba ni msaliti na yule aliyesema kuwa CCM haiwezi kustawisha uchumi wa nchi kwa kile alichokiita kuwa ni sera ya kurukaruka.

Mtatiro tarehe 24 Juni, mwaka huu aliwaeleza waandishi wa habari kuwa Serikali ya CCM haina mpango maalum wa kimaendeleo na haina muelekeo.

Aliutaja mradi wa gesi ya Mtwara na kuwaambia wananchi kuwa waliaminishwa na Serikali ya CCM kuwa mradi huo ndio mradi kombozi lakini gia ikabadili angani na kuhamia kwenye mradi wa umeme wa umeme ni mradi wa Stiegler’s Gorge.

Ni Mtatiro huyuhuyu aliyesema kuwa Serikali ya CCM inawauwa Wazee wastaafu kwa kuwacheleweshea pensheni zao ambapo amedai kuwa serikali inasuasa kuwalipa wastaafu zaidi ya 7,000 waliostaafu mwaka 2016 na 2017 ambao wamejazana mitaani bila kulipwa na ihakikishe kuwa wale wengine 3,000 wanaotarajiwa kustaafu mwezi Julai 2018, wanalipwa mafao na pensheni zao.

Yeye ndiye aliyesema kuwa serikali imerejea njia zilezile zilizoliangusha taifa kwenye uchumi kwa kupita kwenye sera za ujamaa ilhali kuwa bunge limevunjwa meno na bajeti siyo rafiki kwa maendeleo.

Ni yeye yule wa Jumatatu ya tarehe 26 Februari, 2018, amelitaja shambulio baya la kisiasa la kuzuia vyama vya siasa visifanye mikutano ya hadhara huku akidai kuwa Katibu wa Itikadi na  Uenezi wa CCM anafanya bila bughudha yoyote ilhali wapinzani wanakamatwa.

Alhamisi ya tarehe 5 Julai, 2018, alitiwa mbaroni na jeshi la Polisi kwa madai ya kuchapisha andiko lililokuwa linamkejeli Rais John Magufuli kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook.

Ujumbe wake wa tahere 10 Julai, 2018 alisema; “Nawaomba wanachama na madiwani wa CUF Tanga, ambao asilimia 99 wamekuwa na msimamo wa kukilinda chama dhidi ya wasaliti wa ndani, waendelee kuwa imara na watulivu wakati masuala haya yakishughulikiwa kwa njia za kutafuta haki ambazo zimo ndani ya uwezo wetu.

“Mapambano ya ndani ya chama chetu, ya kukilinda na kukiokoa chama, yasingelichukua hata siku moja kama yasingelikuwa yanasimamiwa na na kufadhiliwa na CCM, Usalama Wa Taifa, Vyombo Dola, Serikali, Msajili wa Vyama vya Siasa n.k. tena vyombo hivyo vikifanya hivyo usiku na mchana kwa kumtumia Lipumba na genge lake,” aliwahi kusema Mtatiro .

Professa Ibrahimu Lipumba alijiuzu nafasi yake ya uenyekiti ndani ya CUF siku ya Alhamisi tarehe 6 Agosti, 2015 kwa kile alichodai kuwa haungi mkono ujio wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa katika vyama vinanyounda umoja wa katiba (Ukawa).

Ukawa ni muunganiko wa CUF, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi na NRD.

Lipumba alitengua barua yake ya kujiuzulu na kurejea CUF tarehe 8 Juni, 2018, kwa kuandika barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na kuzua mvutano ndani ya chama hicho. kama mwenyekiti kitendo ambacho kimeibua mpasuko ndani ya chama hicho na kusababisha migogoro uliyokiumbisha chama hicho.

Tangu kutokea kwa migogoro hiyo chama hicho kina pande mbili upo ule unaongozwa na Profesa Lipumba na ule unaongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalimu Seif Sharrif Hamad na kupelekea kutoshiriki chaguzi kadhaa za marudio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!