Wabunge wa UKAWA wakitoka bungeni

Ukawa waanza kwa kususa bungeni

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) bungeni wamesusa kushuhudia kuapishwa kwa wabunge wanne. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Leo vikao vya bunge vimeanza Jijini Dodoma ambapo baada ya dua ya ufunguzi, tukio lililofuata lilikua la kuapishwa kwa wabunge hao.

Wabunge hao ambao awali walikuwa upinzani ni Julius Kalanga (Monduli), Timotheo Mzava (Korogwe vijijini), Mwita Waitara (Ukonga) na Zuberi Kuchauka (Liwale).

Wabunge wa CUF kambi ya Prof. Ibrahim Lipumba walisalia ndani ya ukumbi wa bunge wakati wa tukio hilo.

Kelele na vigelegele vilisikika wakati wapinzani wakitoka bungeni ambapo baadhi ya wabunge wa CCM walikwenda kukaa upande wa viti vya upinzani.

Baada ya wabunge hao kuapishwa, wapinzani walirejea bungeni kuendelea na ratiba ya siku.

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) bungeni wamesusa kushuhudia kuapishwa kwa wabunge wanne. Anaandika Dany Tibason, Dodoma ... (endelea). Leo vikao vya bunge vimeanza Jijini Dodoma ambapo baada ya dua ya ufunguzi, tukio lililofuata lilikua la kuapishwa kwa wabunge hao. Wabunge hao ambao awali walikuwa upinzani ni Julius Kalanga (Monduli), Timotheo Mzava (Korogwe vijijini), Mwita Waitara (Ukonga) na Zuberi Kuchauka (Liwale). Wabunge wa CUF kambi ya Prof. Ibrahim Lipumba walisalia ndani ya ukumbi wa bunge wakati wa tukio hilo. Kelele na vigelegele vilisikika wakati wapinzani wakitoka bungeni ambapo baadhi ya wabunge wa CCM walikwenda kukaa upande wa viti vya upinzani.…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram