Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ukatili kijinsia wawekewa mkakati Mwanza
Habari Mchanganyiko

Ukatili kijinsia wawekewa mkakati Mwanza

Waziri wa Mambo ya Nje ya Serikali wa Jamhuri ya Ireland, Ciaran Cannon, akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa mpango wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia
Spread the love

SERIKALI ya Jamhuri ya Ireland kupitia Shirika la Maendeleo nchini humo (IrishAid), limetoa msaada msaada wa Euro 350,000 sawa na Sh. milioni 750 kwa Shirika lisilo la kiserikali la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (Kivulini) mkoani Mwanza kwa ajili ya kuendeleza mapambano ya vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata 10 wilayani Misungwi, anaandika Moses Mseti.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015/ 2016, vitendo vya ukatili wa kinjisia nchini ni asilimia 58, hatua inayochangia kukwama shughuli za maendeleo kwenye jamii kusuasua.

Msaada huo umetolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland anayeshughulika na masuala ya maendeleo, Ciaran Cannon, aliyeambatana na Mkurugenzi mkuu wa shirika la Maendeleo nchini humo, Ruairi De Burca pamoja na Balozi wa Ireland nchini, Paul Sherlock.

Waziri huyo amesema, mwanamke mmoja kati ya wanawake saba nchini amebainika kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, hatua ambayo amesema inazidi kuchangia kupunguza nguvu kazi ya taifa huku akiwataka wanaume kuacha vitendo hivyo.

Cannon amesema serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali ikiwemo ya kupambana na vitendo vya ukatili, afya na mfuko wa kusadia kaya masikini nchini (Tasaf) ili kuleta mambadiliko katika nyanja ya kiuchumi na mahusiano.

“Zaidi ya asilimia 40 ya wanawake nchini wamebainika kufanyiwa vitendo vya ukatili, hali hii ya ukatili haiwakumbi wanawake pekee bali hata wanaume itawakumba kwa sababu hata shughuli za maendeleo kwenye familia zao hazitakuwa nzuri,” amesema

“Vijana wote mliopo hapa kuweni mfano wa kuigwa wa kwenda kupambana na vitendo vya ukatili majumbani kwenu kwa kuhakikisha mnavitokomeza vitendo hivyo,” amesema Cannon.

Cannon aligusia suala la mimba za utotoni nchini ambapo pia amesema wamejipanga kuhakikisha wanapambana na tatizo hilo.

Amepongeza shirika la Kivulini kwa kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili katika mikoa ya kanda ya ziwa, licha ya changamoto wanazokutana nazo huku akisema kwamba fedha wanazotoa zinafanya kazi nzuri na kuleta matokeo chanya.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mbali na kuwaonya watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa kuwataka kuacha mara moja, amesema Ireland na Tanzania wamekuwa na urafiki wa muda mrefu tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kwamba wameendelea kuchangia katika mfuko wa bajeti ya afya (Basket Fund).

Mkurugenzi wa Kivulini, Yasini Ally amesema Wilaya ya Misungwi ilikuwa ikikabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake ikiwamo kunyanyaswa na waume zao ambapo walipambana na sasa vitendo hivyo vimepungua.

“Zamani kabla hatujaanza kuelimisha wananchi vitendo vya ukatili katika kata tano tulizoanza nazo Misungwi ilikuwa asilimia 56 kwa mwaka 2015/ 2016 na sasa (2017) vimepungua mpaka asilimia 36 na katika hilo tumeokoa mali zenye thamani ya Sh. Biloni 1.1 ambazo wanawake walitaka kudhulumiwa na waume zao,” amesema Ally.

Kata 10 zitakazo nufaika na mradi huo ni Usagara, Idetemya, Kolomije, Igokelo, Misungwi, Mbarike, Misasi, Mabuki, Nhundulu na Sumbugu ambapo watu watafikiwa moja kwa moja kupitia midahalo na mikutano.

Watu 144, 744 watafikiwa huku wengine 289, 488 watapata taarifa kwa kusoma machapisho na kupitia vyombo vya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!