Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ujumbe mzito wa Mbowe kabla ya hukumu
Habari za SiasaTangulizi

Ujumbe mzito wa Mbowe kabla ya hukumu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

IKIWA zimesalia saa kadhaa kwa viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuhukumiwa katika Kesi ya Jinai Na. 112/2018, inayowakabili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wametoa waraka mzito. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Katika nyakati tofauti kupitia kurasa zao za Twitter, viongozi hao wametuma ujumbe wakiwataka wanachama wao kusonga mbele katika harakati za kutetea demokrasia, iwapo watakutana na hukumu ya kifungo jela.

Freeman Mbowe, Mwneyekiti wa Chadema, amesema iwapo watahukumiwa kifungo jela, wafuasi wake wasivunjike moyo.

”Tunakwenda kwenye hukumu ya kesi inayotukabili ya Mauwaji ya Akwilina,ikitokea mimi Freeman Mbowe na wenzangu tumehukumiwa kifungo Jela,naomba wanachadema popote mlipo msivunjike Moyo na wala msirudi nyuma,songeni mbele kwenye mapambano dhidi ya Udhalimu,” amesema Mbowe.

Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), amewaaga rasmi wanachama wa chama hicho, akisema kwamba amejiandaa kwa lolote,  akidai kwamba chochote kinaweza kutokea katika maamuzi ya kesi hiyo.

Maneno ya Halima haya hapa chini

“Wakuu salaam!! Kesho Asubuhi (leo) ni siku ya hukumu ya kesi ya viongozi wa CHADEMA na mimi nikiwa mmoja wapo.

“hochote kinaweza kutokea !!Nimewiwa kutumia nafasi hii kuwaaga rasmi. Itoshe tu kusema, binafsi nimejiandaa kiroho safi kabisa na kukubaliana na chochote kitakacho kuja.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!