Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ujerumani yaipa Tanzania Bil 32
Habari Mchanganyiko

Ujerumani yaipa Tanzania Bil 32

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imepatiwa msaada wa Sh. 32.74 bilioni kutoka Ujerumani kwa ajili ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi, pamoja na kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (V.V.U) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Fedha hizo zimetolewa na Ujerumani kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa ‘Tumaini la Mama’ unaotoa huduma kwa kina mama na watoto wanaotoka kwenye kaya masikini, unaotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Mkataba wa msaada huo ulisainiwa jana tarehe 9 Septemba 2019 jijini Dar es Salaam na Doto James , Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Dk. Annika Calov, Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, James amesema sehemu ya fedha hizo zitatumika kununua vifaa tiba vinavyohusiana na afya ya uzazi kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika mikoa iliyochaguliwa kunufaika na mradi huo.

 Dk. Calov amesema fedha hizo zitasaidia kuboresha afya ya mama na mtoto pamoja na kuzia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda na mtoto katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Tanga, Lindi na Mtwara.

Kwa upande wake Bernard Konga, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF amesema tangu mradi huo uanze mwaka 2012, kina mama 1,157,191 wamenufaika nao kwa kuwa na bima ya afya kupitia shirika hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!