Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Uhuru vyombo vya habari wahojiwa bungeni
Habari Mchanganyiko

Uhuru vyombo vya habari wahojiwa bungeni

Spread the love

MALALAMIKO ya kuminywa kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini, yameibuka tena leo tarehe 18 Aprili 2019 bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akichangia Bajeti ya Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2018/19, Khatibu Said Haji, Mbunge wa Konde (CUF) amempinga Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kauli yake kwamba, Tanzania inasifiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari. 

“Juzi nilimsikia Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Kabudi akiisifia nchi yetu juu ya mafanikio makubwa na sifa waliyiopata duniani kuhusu uhuru wa vyombo habari.

“…Ni pamoja na kuwa na idadi kubwa ya magazeti, kwa hiyo ilikuwa sifa kubwa kwa nchi yetu…., siku mbili baadaye nimemsikia Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Abbas (Hassan Abbas) akitaka magazeti yaliyoripoti taarifa za uchambuzi wa taarifa aliyoitoa kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, waende wakajieleze kwa namna walivyochambua taarifa hizo,” amesema Khatibu.

Amehoji sababu za sifa aliyoieleza Prof. Kabudi kutoka nje na taarifa iliyotolewa na CAG na kuchambuliwa kisha Dk. Abbas kutaka vyombo hivyo vijieleze.

Amehoji uhuru wa vyomvo vya habari, ambapo hata zile habari zilizo wazi, zikiandikwa wahariri wanatakiwa kujieleza. “sasa tunasifiwa kwa lipi na tunarudi tunafanya nini.?” Amehoji.

“Vyombo vya habari vinatakiwa vijieleze, kosa lao lipi? kwani wanalipwa mishahara kwa kutegemea kazi zao zinavyotoka na kuwajulisha Watanzania kipi kinaendelea katika nchi,’ amesema.

Devotha Minja, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) amesema, kuwa na vyombo vingi vya habari sio kigezo cha uhuru wa habari akifafanua kwamba, vyombo hivyo vinafanyaje kazi?

Amesema, kukosekana kwa uhuru wa vyombo habari kunaanzia ndani ya ukumbi wa Bunge, kutokana na wabunge kutotendewa haki.

Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge wa Mbeya Mjini amesema, hata kitendo cha kukataa hotuba za upinzani, ni shambulio la uhuru wa vyombo vya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!