MAJINA ya watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi nchini, waliomwandikia Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga yameanza kutajwa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Tayari Dk Ringo Tenga, Mkurugenzi na Mwanasheria wa Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited, ni miongoni mwa watuhumiwa ambao tayari wameandika barua ya kukiri na kuomba afueni.
Byrson Shayo ambaye ni wakili wa Dk. Tenga leo tarehe 27 Septemba 2019, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati ilipotajwa kesi hiyo.
Dk. Ringo akiwa na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka sita ikiwa ni pamoja na tuhumza za utakatishaji fedha jambo lililoisababisha hasara Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) hasara zaidi ya Dola za Marekani 3,748,751.
Watuhumiwa wengine ambao wamemwandiki barua DPP ni pamoja na Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo.
Kwa mara ya kwanza Dk. Tenga na wenzake walifikisha mahakamani tarehe 20 Novemba 2017 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Leave a comment