Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni

Uhifadhi magereza ni kwa mujibu wa sheria – Masauni

SERIKALI imesema, moja ya jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapokea na kuwaifadhi waharifu wa aina zote, wanaopelekwa kwa mujibu wa sheria. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa leo tarehe 13 Septemba 2019 bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipojibu swali na mbunge wa viti maalum, Nagma Giga (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali haioni kuweka pamoja wafungwa na watuhumiwa ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao ya baadaye.

Pia alitaka kujua, je serikali haioni imepoteza nguvu kazi ya vijana kwa kuwachanganya na wale wabakaji hususani vijana kuanzia miaka 18 hadi 30?

Akijibu swali hilo Masauni amesema, moja ya majukumu ya jeshi la magereza ni kuwapokea na kuwahifadhi magerezani wahalifu wa aina zote kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Amesema, sanjari na hilo kanuni za uendeshaji wa Magereza za mwaka 1967 zinaelekeza, uhifadhi wa waharifu utafanyika kwa kuzingatia utenganisho kwa vigezo vya jinsia, umri, kosa na Mifungo.

SERIKALI imesema, moja ya jukumu la Jeshi la Magereza ni kuwapokea na kuwaifadhi waharifu wa aina zote, wanaopelekwa kwa mujibu wa sheria. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). Kauli hiyo ilitolewa leo tarehe 13 Septemba 2019 bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipojibu swali na mbunge wa viti maalum, Nagma Giga (CCM). Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali haioni kuweka pamoja wafungwa na watuhumiwa ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao ya baadaye. Pia alitaka kujua, je serikali haioni imepoteza nguvu kazi ya vijana kwa kuwachanganya na wale wabakaji hususani vijana kuanzia miaka 18 hadi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram