Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ugonjwa wa Lissu: Mahakama yaahirisha kesi
Habari Mchanganyiko

Ugonjwa wa Lissu: Mahakama yaahirisha kesi

Tundu Lissu, Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha kesi inayowakabili wahariri wa Gazeti la Mawio, kutokana na kuumwa kwa mshitakiwa wa nne (Tundu Lissu). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mshitakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo ni Jabir Idrisa, mwandishi mwandamizi wa gazeti hilo, mshitakiwa wa pili ni Simon Mkina, Mhariri, Ismail Mahboob, Meneja wa Kampuni ya uchaishaji ya Flint na mshitakiwa wa nne ni Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki.

Lissu yupo nchini Ubelgiji, kwa matibabu ya majeraha yaliyotokana na kushambuliwa kwa risasi terehe 7 Septemba 2017, eneo la Area ‘D’ jijini Dodoma na watu wasiojulikana.

Leo tarehe 24 mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Kisutu, Mdhamini wa Lissu, Robart Katula ameieleza mahakama hiyo kuwa, mdhamana wake yupo nchini Ubelgiji.

Shauri hilo limeahirishwa mpaka tarehe 22 Agosti 2019, kwa ajili ya usikilizwaji.

Watuhumiwa wote wanadaiwa, tarehe 14 Januari 2016 walichapsha habari kwenye gazeti la Mawio, toleo namba 182 la mwaka 2016 iliyodaiwa kuwa ya uchochezi yenye kichwa cha habari ‘Machafuko Yaja Zanzibar’.

Kesi hiyo ilifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Aprili 2016 ambako watuhumiwa wote walikana mashitaka na kupata dhamana.

Hata hivyo imeendelea kuahirishwa kwa miaka miwili baada ya kuwa ilishaanza kusikilizwa kwa upande wa mashitaka kuwaita mashahidi wawili – aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni na Raphael Hokororo, aliyekuwa msaidizi wa mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).

Hokororo aliyekuwa akifanya kazi ya kusajili magazeti nchini, baadaye alikuja kustaafu. Usikilizaji wa kesi ulisita baada ya shambulio la risasi kadhaa za moto dhidi ya Lissu ambalo mwenyewe analieleza kuwa ni jaribio la kumuua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!