April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uganda yapiga marufuku kampeni za majukwaani

Bobi Wine

Spread the love

TUME ya Uchaguzi ya Uganda imepiga marufuku mikusanyiko ya kampeni za jukwaani na kuagiza, kampeni za uchaguzi mkuu zifanyike kupitia vyombo vya habari. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kwenye uchaguzi huo miezi sita ijayo, Uganda inatarajia kuchagua rais, wabunge na wawakilishi wa ngazi za chini. Uchaguzihuo unatarajiwa kufanyika Januari 2021.

Tume hiyo imeeleza, imechukua hatua hiyo kuhakikisha virusi vya corona havipati nafasi ya kusambaa kutokana na mikusanyiko hiyo, hivyo kuliingiza taifa kwenye janga.

Taarifa ya tume hiyo imeeleza, utaratibu wa sasa wa uvaaji barakoa, umbali unakubalika na njia zingine zinazotumika kujiepusha na maambukizi hayo, zitasimamiwa siku ya upigaji kura.

error: Content is protected !!