May 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ugaidi: IGP Sirro kukutana na IGP wa Msumbiji

IGP Simon Sirro

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Simon Sirro anatarajiwa kufanya mazungumzo na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji, Bernadino Rafael kuhusu hali ya usalama wa mataifa hayo mawili. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania kupitia ukurasa wake wa Twitter, kikao hicho cha IGP Sirro na Kamanda Rafael kitafanyika leo Ijumaa tarehe 20 Novemba 2020 mkoani Mtwara.

“IGP Sirro leo anatarajia kukutana na IGP wa nchiya Msumbiji katika kikao kazi cha ujirani mwema baina ya nchi hizo mbili kitakachofanyika mkoani Mtwara,” inaeleza taarifa ya Jeshi la Polisi la Tanzania.

Taarifa hiyo imekuja siku moja tangu IGP Sirro azungumze na wanahabari kuhusu masuala ya usalama yanayoendelea mkoani Mtwara katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mauaji ya raia sambamba na matukio ya utekwaji watu na kuchomwa makazi ya watu katika Kijiji cha Kitaya mkoani humo. Matukio hayo yanadaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa Dola la Kiislamu (IS).

Akizungumzia matukio hayo, IGP Sirro alisema vyombo vya ulinzi na usalama vimepelekwa mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama na kwamba kwa sasa hali vinaendelea vizuri na utekelezaji wa majukumu yao.

Hata hivyo, IGP Sirro alituhumu baadhi ya Watanzania kutoa ushirikiano kwa wanamgambo hao, ikiwemo kuwapa ramani ya maeneo kufanya uharibifu.

IGP Sirro alisema, Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata baadhi ya Watanzania wanaotuhumiwa kuhusika na suala hilo, na kwamba katika mahojiano yao walikiri kuwa na mpango wa kujiunga na kundi la wanamgambo hao.

error: Content is protected !!